Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping ampongeza Putin kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Russia
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amempongeza Vladimir Putin kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Russia akisema katika miaka ya hivi karibuni watu wa Russia wameshikamana na kuwa kitu kimoja, wameshinda changamoto na kupiga hatua thabiti kuelekea maendeleo na ustawishaji wa taifa.
Rais Xi amesema, kuchaguliwa tena kwa Putin kuwa rais wa Russia kunaonyesha kikamilifu uungaji mkono wa watu wa Russia kwake.
Russia hakika itapata mafanikio makubwa zaidi katika maendeleo na ujenzi wa taifa chini ya uongozi wa Putin, Rais Xi amesema.
Huku akisisitiza kuwa China inatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia, Rais Xi amesema China iko tayari kudumisha mawasiliano ya karibu na Russia ili kuhimiza maendeleo endelevu, mazuri, thabiti na ya pande zote ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote wa China na Russia kwa zama mpya ili kunufaisha nchi hizo mbili na watu wake.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma