Lugha Nyingine
Eneo la kuzalisha umeme kwa nishati mbalimbali lililoko Kusini Magharibi mwa China lazalisha umeme zaidi ya trilioni 1 kWh
Picha iliyopigwa Novemba 2, 2022 ikionyesha kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji katika Vituo vya Kuzalisha Umeme kwa Nishati za Maji, Upepo na Jua kwenye eneo la mtiririko wa Mto Yalong, katika Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China. (Kampuni ya Uzalishaji Umeme kwa Maji ya Mto Yalong / Xinhua)
CHENGDU – Kampuni ya Uzalishaji wa Umeme wa Yalong imesema kuwa, hadi kufikia Alhamisi, Vituo vya Kuzalisha Umeme kwa Nishati za Maji, Upepo na Jua la Bonde la Mto Yalong kilichoko katika eneo la mtiririko wa Mto Yalong, Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China vilikuwa vimezalisha umeme wa kilowati-saa (kWh) zaidi trilioni 1 tangu vilipoanzishwa.
Nishati safi iliyozalishwa kwenye eneo hilo katika miongo miwili iliyopita imesaidia kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni yenye uzito wa takriban tani milioni 800, sawa na upunguzaji wa hewa ya eneo la miti iliyopandwa kwenye ardhi yenye ukubwa wa hekta milioni 8, imesema kampuni hiyo, ambayo ni mjenzi na mwendeshaji wa mradi huo.
Kituo cha kwanza cha kuzalisha umeme kwenye eneo hilo kilianzishwa na kufanya kazi Mwaka 1998, sasa vituo saba vya kuzalisha umeme kwa nishati ya maji na vingine vitano vya kuzalisha umeme kwa nishati za upepo na jua vinavyofanya kazi vimekuwa na uwezo wa jumla wa kuzalisha umeme wa takriban kilowati milioni 21.
Kwa sasa, vituo vya eneo hilo vinaweza kuzalisha umeme wa takriban kWh bilioni 90 kwa mwaka. Miradi yote inayojengwa imepangwa kukamilika ifikapo Mwaka 2035, huku ikiwa na makadirio ya kuzalisha umeme wa kufikia takriban kWh bilioni 200 kwa mwaka, kampuni hiyo imesema.?
Picha iliyopigwa Novemba 25, 2022 ikionyesha kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji katika Vituo vya Kuzalisha Umeme kwa Nishati za Maji, Upepo na Jua kwenye eneo la mtiririko wa Mto Yalong, katika Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China. (Kampuni ya Uzalishaji Umeme kwa Maji ya Mto Yalong / Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma