Lugha Nyingine
Kijiji cha Longwangba kikichokuwa maskini kupindukia, chachangia simulizi na Dunia kuhusu mageuzi ya kijani na kutokomeza umaskini
Picha hii iliyopigwa Februari 2024 ikionyesha bidhaa maaulum za kilimo za kienyeji na bidhaa za urithi wa utamaduni usioshikika kutoka Kijiji cha Longwangba, kijiji kilicho kaskazini-magharibi mwa China, zikionyeshwa kwenye Maonyesho ya 60 ya Kimataifa ya Kilimo huko Paris, Ufaransa. (Xinhua)
YINCHUAN - Kijiji cha Longwangba cha Xihaigu, katika Mji wa Guyuan katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia, Kaskazini-Magharibi mwa China ambacho kiko katika eneo lililotangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa "eneo lisilofaa kukaliwa na binadamu", kimepata pongezi za kimataifa kwa sababu ya mageuzi yake ya kijani ambapo mwakilishi wa kijiji hicho hivi karibuni aliwasilisha simulizi ya mafanikio ya kijiji hicho kwenye Maonyesho ya 60 ya Kimataifa ya Kilimo huko Paris, Ufaransa.
"Nilifurahi kuchangia simulizi ya ustawishaji wa kijiji chetu na mafanykio ya kiikolojia nchini China na watu wa Ufaransa na Dunia," Jiao Jianpeng, naibu mkuu wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ya Longwangba amesema.
Jiao alipeleka bidhaa maalum za kilimo za kienyeji kwenye maonyesho hayo, ikiwa ni pamoja na matunda ya goji, mtama, na juisi ya parsley, pamoja na bidhaa za urithi wa utamaduni usioshikika kama vile kazi za sanaa ya kukata karatasi, vikaragosi vya kivuli na vipodozi vya uso.
Juisi ya parsley huenda haipendezi kwa kuisikia, lakini ilipata shabiki wake Daniel Vial, ambaye alitunukiwa nishani ya Chevalier de la Légion d'Honneur na rais wa zamani wa Ufaransa. Vial alipotembelea banda la Jiao, alijaribu juisi hiyo, akaipiga kidole gumba na kusema "Ladha ya ajabu!"
Bidhaa hizo zilizoonyeshwa zilipendwa sana miongoni mwa watembeleaji wa maonyesho hayo, ambapo mauzo yalizidi Yuan 400,000 (kama dola 56,367 za Kimarekani) katika siku chache tu. Baada ya kurudi nyumbani, Jiao bado anapokea maulizo ya ununuzi kutoka kwa wateja wa Ufaransa.
Si muda mrefu uliopita, Wilaya ya Xihaigu, ambako Kijiji cha Longwangba kilichopo, ilikuwa mojawapo ya maeneo yenye umaskini zaidi nchini China, huku asilimia zaidi ya 80 ya watu wakiishi chini ya mstari wa umaskini wakati wa hatua ya awali ya kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango ya China.
Katika eneo la Xihaigu lenye uhaba wa maji, rasilimali za maji kwa kila mtu zilikuwa chini ya asilimia 8 ya kiwango cha wastani cha China. Ilitangazwa kuwa "eneo lisilofaa kukaliwa na binadamu" na wataalam wa Umoja Mataifa Mwaka 1972.
Hali ngumu ya mazingira ya asili ilifanya binadamu kuishi na kustawi kuwa vigumu sana. Lakini mazingira ya kiikolojia huko Xihaigu yameboreka hatua kwa hatua kwa sababu ya mfululizo wa mipango ya ulinzi wa ikolojia, kama vile Mpango wa Ukanda wa Misitu wa Mikoa Mitatu ya Kaskazini mwa China. Huko Guyuan, kiwango cha uwepo wa misitu kimeongezeka kutoka asilimia 1.4 mwishoni mwa miaka ya 1970 hadi asilimia 27.28 Mwaka 2022.
Juhudi za China za kupunguza umaskini pia zimeboresha miundombinu ya Longwangba, ikiwa ni pamoja na barabara, umeme, nyumba na maji safi.
Mwaka 2023, Longwangba ilipokea watalii zaidi ya 410,000, huku mapato yatokanayo na utalii yakifikia yuan milioni 19.41. Kupitia njia mbalimbali za maendeleo kama vile utalii na afya, wastani ya mapato ya kila mwaka kwa wanavijiji yameongezeka kutoka chini ya yuan 2,300 Mwaka 2012 hadi yuan 15,500 Mwaka 2023.
Kutoka kijiji "kisichofaa kukaliwa na binadamu" hadi "chenye maendeleo ya kijani, kiikolojia na yenye ubora wa hali ya juu," Longwangba imekuwa kielelezo cha China katika kuondoa umaskini na ustawishaji wa kijiji.
Picha iliyopigwa Julai 2021 ikionyesha Kijiji cha Longwangba katika Wilaya ya Xiji, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia, Kaskazini-magharibi mwa China. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma