Lugha Nyingine
Huawei yatoa mafunzo ya ujuzi wa kidijitali kwa vijana zaidi ya 240 kaskazini mwa Uganda
Kampuni ya teknolojia ya China Huawei imetoa mafunzo kwa vijana 241 katika wilaya ya Alebtong, kaskazini mwa Uganda, na kuwapa ujuzi mbalimbali wa kidijitali.
Huawei imesema katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu wiki hii kwamba vijana hao walihitimu Machi 7 baada ya mafunzo ya wiki tatu.
Denis Obua, afisa mwandamizi wa chama tawala nchini Uganda cha National Resistance Movement (NRM), ameipongeza Huawei kwa kutekeleza mpango huo wa mafunzo unaojulikana kwa jina la DigiTruck, unaoendana na mpango wa maendeleo wa nchi hiyo.
DigiTruck, ambalo ni lori lililobadilishwa kuwa darasa la mafunzo ya kompyuta, husafiri kutoka mkoa mmoja hadi mwingine, ambapo wakufunzi hufundisha watu biashara ya mtandaoni na utafiti kuhusu mtandao wa intaneti. Ni sehemu ya mpango wa TECH4ALL wa Huawei wa kuhimiza maendeleo ya kidijitali yaliyo jumuishi na endelevu kote duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma