Lugha Nyingine
Mauzo ya magari ya China yaongezeka kwa asilimia 11.1 katika miezi miwili ya kwanza ya Mwaka 2024
Picha hii iliyopigwa tarehe 11 Oktoba 2023 ikionyesha Kiwanda cha Pili wa Uundaji wa Magari cha Kampuni ya Mgari ya NIO huko Hefei, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (Xinhua)
BEIJING - Takwimu kutoka Shirikisho la Viwanda vya Magari la China zilizotolewa siku ya Jumatatu zinasema, mauzo ya magari ya China yameongezeka kwa asilimia 11.1 hadi kufikia magari milioni 4.03 katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu, yakilinganishwa na yale ya kipindi kama hicho mwaka jana.
Uzalishaji wa magari nchini katika kipindi cha Januari-Februari umeongezeka kwa asilimia 8.1 mwaka hadi mwaka hadi kufikia magari milioni 3.92, kwa mujibu wa shirikisho hilo.
Hasa, uzalishaji na mauzo ya magari ya abiria vilifikia magari milioni 3.36 na milioni 3.45, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.9 na asilimia 10.6 mwaka hadi mwaka, mtawalia, takwimu hizo zimeonyesha.
Uzalishaji wa magari ya kibiashara uliongezeka kwa asilimia 9 mwaka hadi mwaka kufikia magari 560,000, huku mauzo ya magari hayo yakiongezeka kwa asilimia 14.1 na kufikia magari 575,000.
Sekta ya magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) ilidumisha kasi ya ukuaji wa haraka katika kipindi cha miezi hiyo miwili. Uzalishaji wa NEVs nchini China ulifikia magari milioni 1.25, ukiongezeka kwa asilimia 28.2 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Mauzo ya NEVs yaliongezeka kwa asilimia 29.4 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana na kufikia magari milioni 1.21.
Mauzo ya jumla ya magari ya China kwa nchi za nje yalifikia magari 822,000 katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la asilimia 30.5 mwaka hadi mwaka.
Mauzo ya magari ya China yalifikia magari takriban milioni 1.58 mwezi Februari pekee, ikiwa imepungua kwa asilimia 19.9 kutoka kipindi kama hicho mwaka mmoja uliopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma