Lugha Nyingine
Benki ya Maendeleo ya China yaongeza uungaji mkono kwa ukarabati wa maeneo ya hali duni mijini
Picha hii iliyopigwa Novemba 25, 2022 ikionyesha muonekano wa jumuiya ya makazi ya Bada baada ya kukarabatiwa na kuboreshwa katika Eneo la Xixiu la Mji wa Anshun, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Li Jingya)
BEIJING - Benki ya Maendeleo ya China (CDB) ambayo ni benki muhimu ya kuhimiza utekelezaji sera za uchumi nchini humu, imeongeza uungaji mkono wa kutoa mkopo kwa miradi ya ukarabati wa maeneo yenye hali duni mijini kote nchini China ambapo hadi kufikia Alhamisi wiki iliyopita, benki hiyo ilikuwa imetoa yuan bilioni 61.4 (kama dola bilioni 8.65) za mikopo maalum kwa miradi 271 katika miji 33 ikiwemo Beijing, Shanghai, Guangzhou na Wuhan, takwimu kutoka benki hiyo zinaonyesha.
Miradi hii imenufaisha kaya zipatazo 360,000 na imesaidia ujenzi wa nyumba 695,000 za watu waliolazimika kuachana na makazi yao ya awali kutokana na mageuzi ya muundo wa mijini, CDB imesema.
Benki hiyo imeongeza kuwa ilitoa sehemu ya kwanza ya mikopo hiyo Januari 30 mwaka huu, ambayo imefikia thamani ya yuan bilioni 9.08.
Mkutano wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu kazi ya uchumi, ambao ulifanyika Desemba mwaka jana na kuweka vipaumbele vya sera ya uchumi nchini China kwa mwaka 2024, ulisisitiza juhudi za kuendeleza ujenzi wa nyumba za bei nafuu na miundombinu ya umma kwa matumizi ya kawaida na ya dharura, pamoja na ukarabati wa maeneo yenye hali duni mijini.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma