Lugha Nyingine
Akiba ya fedha za kigeni ya China yaongezeka hadi kufikia dola za Kimarekani trilioni 3.2258
Picha ya data ikionyesha mfanyakazi akihesabu dola za Marekani kwenye benki moja katika Wilaya ya Tancheng ya Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua/Zhang Chunlei)
BEIJING – Takwimu zilizotolewa na Idara ya kitaifa ya usimamizi wa fedha za kigeni zimeonesha kuwa, Akiba ya jumla ya fedha za kigeni ya China imefikia dola trilioni 3.2258 za Kimarekani hadi kufikia mwisho wa Februari mwaka huu, ambayo ongezeko lake limefikia dola bilioni 6.5 yaani 0.2% ikilinganishwa na mwisho wa Januari.
Katika taarifa yake, idara hiyo imesema kuwa, ikiwa imeathiriwa na takwimu za uchumi na matarajio ya sera za fedha za nchi zenye uchumi mkubwa, fahirisi ya dola iliongezeka huku bei za mali za kifedha duniani zikiwa mchanganyiko.
Idara hiyo imehusisha ongezeko hilo la kiwango cha akiba ya fedha za kigeni nchini China na athari za pamoja za tafsiri ya sarafu na mabadiliko ya bei ya mali na mambo mengine.
Idara hiyo imeongeza kusema kuwa, uchumi wa China utaendelea kuimarika, hii itasaidia kudumisha hali ya utulivu wa jumla kwa kiwango cha akiba ya fedha za kigeni.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma