Lugha Nyingine
China yalenga ukuaji wa uchumi wa karibu asilimia 5 kwa mwaka huu
Kikao cha ufunguzi cha mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China Machi 5, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
Ripoti ya kazi ya serikali iliyowasilishwa Jumanne kwenye kikao cha mkutano unaoendelea wa Bunge la Umma la China kwa ajili ya kujadiliwa, inasema China inalenga ukuaji wa uchumi wa karibu asilimia 5 kwa mwaka huu.
China inatarajia kuunda nafasi za ajira zaidi ya milioni 12 katika maeneo ya mijini na kuweka kiwango cha ukosefu wa ajira mijini katika karibu asilimia 5.5, kwa mujibu ripoti hiyo.
Ripoti inasema sera za bajeti zinazochochea hamasa na sera makini za fedha zitaendelea, huku uwiano wa nakisi kwa pato la taifa (GDP) ukiwekwa kuwa asilimia 3 na nakisi ya serikali ikiongezeka kwa yuan bilioni 180 kutoka kwenye kiwango cha bajeti ya 2023.
China pia imepanga kutoa Yuan trilioni 3.9 za dhamana maalum kwa serikali za mitaa, ikiwa ni ongezeko la Yuan bilioni 100 kutoka kiwango cha mwaka jana.
Serikali pia itatoa hati fungani maalum za muda mrefu zaidi katika kila miaka kadhaa ijayo kwa madhumuni ya kutekeleza mikakati mikuu ya kitaifa, na kujenga uwezo wa kiusalama katika maeneo muhimu, ikianza kwa kutoa hati fungani yenye thamani ya Yuan trilioni 1 mwaka huu, ripoti hiyo imesema.
Ripoti pia imesema uthabiti wa mwelekeo wa sera ya jumla unapaswa kuimarishwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma