Lugha Nyingine
Mji Mkuu wa uzalishaji wa magari ya RV wa China wasajili ongezeko la asilimia 17.8 la uuzaji nje wa RV kwa Mwaka 2023
Picha iliyopigwa Agosti 10, 2023 ikionesha Magari ya safari za mapumziko na malazi (RVs) yanayoundwa na kampuni ya magari yanayotumia nishati mpya ya Rongcheng Compaks katika Mji wa Rongcheng, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua/Li Zhihao)
Mji wa Rongcheng katika Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, ambao ni kituo kikubwa wa uundaji na uuzaji nje ya nchi wa Magari ya safari za mapumziko na malazi (RV) nchini China, umesajili thamani ya uuzaji nje ya nchi wa magari ya RV ya yuan bilioni 1.82 (takriban Dola bilioni 256 za Kimarekani) mwaka 2023, ikiashiria ongezeko la asilimia 17.8 kutoka kiwango cha mwaka uliotangulia, kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa.
Mnamo mwaka 2022, Rongcheng iliuza nje ya nchi magari ya RV 17,173, ikiwakilisha asilimia 57.5 wa mauzo yote ya nje ya RV ya China, na uzalishaji wake wa magari ya RV, kwa jumla 17,475, ulichukua asilimia zaidi ya 30 ya ujumla ya China, takwimu kutoka Idara ya Habari na Teknolojia ya Viwanda ya Rongcheng zinaoensha. Wanunuzi wake wakuu ni pamoja na Australia, New Zealand, Marekani, kati ya nchi na maeneo mengine.
Liu Shaoxun, meneja mkuu wa Kampuni ya magari yanayotumia nishati mpya ya Rongcheng Compaks iliyoko Mji wa Rongcheng amehusisha ongezeko hilo la mauzo ya nje ya RV katika mji huo Mwaka 2023 na mnyororo wake kamilifu wa viwanda unaojikita katika magari ya RV. Takwimu kutoka Idara ya Habari na Teknolojia ya Viwanda ya Rongcheng zinaoensha, kuna kampuni 10 za uundaji magari ya RV zenye ukubwa juu ya kigezo mjini Rongcheng, na kampuni zaidi ya 50 zinazozalisha vipuri na sehemu za magari ya RV.
Picha iliyopigwa tarehe 18, Februari 2024 ikionesha wafanyakazi wakiunda magari ya RV katika kiwanda cha Kampuni ya magari yanayotumia nishati mpya ya Rongcheng Compaks huko Rongcheng, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua/Li Zhihao)
Picha iliyopigwa tarehe 18, Februari 2024 ikionesha mfanyakazi akiunda magari ya RV katika kiwanda cha Kampuni ya magari yanayotumia nishati mpya ya Rongcheng Compaks huko Rongcheng, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua/Li Zhihao)
Picha iliyopigwa tarehe 10, Agosti 2023 ikionesha magari ya RV yaliyoundwa na Kampuni ya magari yanayotumia nishati mpya ya Rongcheng Compaks huko Rongcheng, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua/Li Zhihao)
Sherehe kwenye hekalu zafanyika Mkoa wa Henan katikati ya China
Boti nyingi zafanya safari baharini katika Mji wa Sanya, Mkoani Hainan, China
Sherehe ya "Kuonyesha Buddha" yafanyika katika Hekalu Kaskazini Magharibi mwa China
Watu wa kabila la Wagelao washerehekea Sikukuu ya Maolong huko Guizhou, Kusini Magharibi mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma