Lugha Nyingine
Kampuni za China zashinda zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya mafuta ya petroli kwenye Bandari ya Dar es Salaam
Picha hii iliyopigwa Desemba 29, 2023 ikionyesha bandari ya Dar es Salaam wakati wa machweo mjini Dar es Salaam, Tanzania. (Xinhua/Wang Guansen)
Kampuni mbili za China zimeshinda zabuni kujenga matangi na miundombinu husika kwa ajili ya kupokea, kuhifadhi na kusambaza mafuta ya petroli na bidhaa za nishati katika Bandari ya Dar es Salaam, amesema ofisa mwandamizi wa Tanzania.
Kampuni hizo mbili, ambazo ni Shirika la Uhandisi wa Daraja Kuu la Reli la China na Kampuni ya Uhandisi ya Wuhan zimetangazwa na Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Makame Mbarawa siku ya Jumatatu.
Mbarawa amesema kuwa mradi huo wenye thamani ya shilingi za Tanzania bilioni 678.6 unaashiria jududi mpya ya serikali katika kuimarisha ufanisi wa kushughulikia mizigo katika bandari kuu ya nchi hiyo.
Mradi huo utahusisha ujenzi wa matangi 15 yenye uwezo wa jumla wa kuhifadhi bidhaa za petroli zenye mita za ujazo 420,000. Mbarawa ameongeza kuwa mradi huo umepangwa kumalizika ujenzi wake ndani ya miaka miwili.
Plasduce Mbossa, mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) amesema kuwa mradi huo utakapokamilika, upakuaji wa bidhaa za petroli utapungua kutoka muda wa sasa wa wastani wa siku 11 hadi 12 hadi siku 3 hadi 4.
Mbossa amesema, ujenzi wa matangi hayo unatarajiwa kuleta manufaa mbalimbali, yakiwemo uwezekano wa kupungua kwa bei ya mafuta, kupunguza tatizo la upotevu wa mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, na kupungua kwa malalamiko miongoni mwa wafanyabiashara wa mafuta.
Ameongeza kuwa ujenzi wa matangi hayo utaboresha ukusanyaji wa ushuru kwa sababu mafuta yote yatapokelewa, kupimwa kwa usahihi katika sehemu moja na chini ya mamlaka ya bandari hiyo kabla ya kusambazwa.
Bandari ya Dar es Salaam (Picha/VCG)
Boti nyingi zafanya safari baharini katika Mji wa Sanya, Mkoani Hainan, China
Sherehe ya "Kuonyesha Buddha" yafanyika katika Hekalu Kaskazini Magharibi mwa China
Watu wa kabila la Wagelao washerehekea Sikukuu ya Maolong huko Guizhou, Kusini Magharibi mwa China
Wakulima kote China wawa na pilika nyingi za uzalishaji wa kilimo wakati Siku ya Yushui yakiwadia
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma