Lugha Nyingine
Bunge la Umma la China lahitimisha mkutano wake wa kamati ya kudumu
BEIJING - Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la 14 la China imehitimisha mkutano wake wa nane siku ya Jumanne mjini Beijing ambapo katika kikao cha kufunga, wajumbe wamepiga kura kupitisha Sheria iliyorekebishwa kuhusu kuhifadhi siri za nchi, na Rais Xi Jinping ametia saini amri ya rais ya kutangaza sheria hiyo.
Zhao Leji, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya bunge hilo la umma, aliongoza mkutano huo wa kufunga.
Wajumbe wamepitisha kimsingi ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China. Baraza la Wenyeviti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China lilipendekeza Zhao Leji kutoa ripoti hiyo kwenye mkutano ujao wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China.
Wajumbe pia wamepitisha ripoti ya kuchaguliwa na kupitishwa kwa wajumbe wa mkutano na miswada mingine inayohusu uteuzi wa maofisa viongozi. Wamepitisha rasimu ya ajenda ya mkutano wa Bunge la Umma la China na rasimu ya orodha ya majina ya wajumbe na katibu mkuu wa kikao, na kuamua kuwasilisha rasimu hizo na kujadiliwa kwenye mkutano wa maandalizi ya mkutano ujao wa Bunge la Umma la China. Pia wamepitisha rasimu ya orodha ya majina ya wajumbe waalikwa wasiopiga kura kwenye mkutano.
Akielezea umuhimu wa mkutano ujao wa Bunge la Umma la China katika hotuba yake kwenye kikao cha kufunga, Zhao ametoa wito wa kufanya maandalizi kwa makini zaidi ili kuhakikisha mkutano unafanyika kidemokrasia, wenye mshikamano, wenye matokeo halisi na wa kuleta maendeleo.
Zhao pia ametoa wito wa kuungwa mkono na kutiwa moyo zaidi kwa wajumbe wa mkutano wa Bunge la Umma la China ili waseme ukweli na kupendekeza suluhu zenye kuleta matokeo halisi, na hivyo kuonesha kikweli sauti na matakwa ya wananchi.
Pia amehimiza kutangazwa kwa habari njema na kusisitiza uthabiti katika kuitisha mkutano huo.
Zhao aliongoza kikao cha Baraza la Wenyeviti kabla ya kumalizika kwa mkutano huo na kuongoza mhadhara wa wajumbe baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Boti nyingi zafanya safari baharini katika Mji wa Sanya, Mkoani Hainan, China
Sherehe ya "Kuonyesha Buddha" yafanyika katika Hekalu Kaskazini Magharibi mwa China
Watu wa kabila la Wagelao washerehekea Sikukuu ya Maolong huko Guizhou, Kusini Magharibi mwa China
Wakulima kote China wawa na pilika nyingi za uzalishaji wa kilimo wakati Siku ya Yushui yakiwadia
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma