Lugha Nyingine
Maofisa Waandamizi wa CPC waripoti kazi kwa Kamati Kuu ya Chama na katibu mkuu Xi
BEIJING - Maofisa Waandamizi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) hivi karibuni wamewasilisha ripoti za kazi zao kwa Kamati Kuu ya Chama na katibu mkuu wake Xi Jinping kwa kufuata kanuni husika zilizowekwa.
Viongozi waliowasilisha ripoti zao ni wajumbe wa Ofisi ya Siasa na Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, na wajumbe wa vikundi vya uongozi wa Chama vya Bunge la Umma la China, Baraza la Serikali la China, na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, pamoja na makatibu wa vikundi vya uongozi wa Chama vya Mahakama Kuu ya Umma ya China na Idara kuu ya Uendeshaji wa Mashtaka ya China.
Baada ya kusoma ripoti zao za kazi, Rais Xi amewataka kuweka mkazo zaidi katika kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, kutekeleza vizuri majukumu yao ya kazi, kuimarisha hisia zao za uwajibikaji wa kisiasa, na kufanya juhudi kubwa kwa mshikamano kwa ajili ya kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu na kusukuma mbele maendeleo ya Ustawishaji wa Taifa la China.
Akieleza kuwa mwaka huu ni mwaka wa 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China na mwaka muhimu wa kutimiza malengo na majukumu yaliyoainishwa katika Mpango wa 14 wa Miaka Mitano wa China (2021-2025), Rais Xi amesisitiza haja ya kutekeleza kikamilifu misingi ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC na mkutano wa pili wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC.
Xi amewataka maofisa hao waandamizi wa Chama wawe watangulizi katika kuimarisha na kupanua matokeo yaliyopatikana katika kampeni ya elimu ya Chama kizima, kutekeleza kikamilifu na kwa kutii dhana mpya ya maendeleo kwa pande zote, na kuendeleza mageuzi kwa kina katika maeneo mbalimbali.
Rais Xi amesema, ni lazima kufanya juhudi katika kudumisha na kuimarisha uchumi unaokua na kuboresha zaidi ustawi wa watu.
Boti nyingi zafanya safari baharini katika Mji wa Sanya, Mkoani Hainan, China
Sherehe ya "Kuonyesha Buddha" yafanyika katika Hekalu Kaskazini Magharibi mwa China
Watu wa kabila la Wagelao washerehekea Sikukuu ya Maolong huko Guizhou, Kusini Magharibi mwa China
Wakulima kote China wawa na pilika nyingi za uzalishaji wa kilimo wakati Siku ya Yushui yakiwadia
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma