Lugha Nyingine
Mwanasayansi wa China alitunukiwa tuzo kwa kazi ya msingi katika upandikizaji sehemu za mwili, tiba ya seli
Huang Xiaojun akizungumza na mgonjwa katika Hospitali ya Watu ya Chuo Kikuu cha Peking mjini Beijing, China, Julai 6, 2023. (Xinhua/Zhang Yuwei)
SAN ANTONIO, Marekani - Mwanasayansi wa China Huang Xiaojun ameshinda tuzo ya juu ya kimataifa siku ya Ijumaa mjini San Antonio Marekani kwa kazi yake ya msingi inayojulikana kama Protokali ya Beijing katika upandikizaji wa sehemu za mwili na matibabu ya seli.
Profesa huyo mtukufu, Mwanataaluma wa Taasisi Kuu ya Uhandisi ya China na Mkurugenzi wa Taasisi ya Hematology katika Chuo Kikuu cha Peking, amepokea Tuzo Mashuhuri ya kila Mwaka ya Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Damu na Uboho (CIBMTR) kwenye Mikutano ya Tandem ya Mwaka 2024.
Mikutano hii huchukuliwa kama jukwaa la wataalam wakuu wa kimataifa kuhimiza ushirikiano maarifa muhimu yanayojikita katika kuimarisha na kuhifadhi maisha ya watu wanaokabiliana na matatizo yanayohusiana na damu.
"Nimeheshimiwa sana," amesema Huang katika hotuba yake. "Nataka kusema tuzo hii siyo tu heshima kubwa kwangu, lakini pia ni uthibitisho wa timu yangu, na hata motisha zaidi kwa maendeleo ya haraka ya upandikizaji wa seli ya shina ya damu nchini China."
Huang alianzisha msururu wa mbinu muhimu za upandikizaji wa seli za damu zinazofanana isiyokuwa ya T iliyopunguzwa, ambayo polepole ilikuja kuwa Protokali ya Beijing ya G-CSF/ATG, na kuongeza muda wa kuishi kwa miaka 3 kutoka asilimia takriban 20 hadi asilimia karibu 70 kwa wagonjwa saratani ya damu wanaopata matibabu ya upandikizaji wa seli hizo, Michael Verneris, mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya CIBMTR, aliuambia mkutano.
Mikutano ya Tandem ya 2024 ya Februari 21-24, iliyoratibiwa kwa pamoja na Jumuiya ya Upandikizaji na Tiba ya Seli ya Marekani na CIBMTR, imevutia maelfu kadhaa ya madaktari, watafiti na wataalamu wa afya kutoka kote duniani.
Sherehe ya "Kuonyesha Buddha" yafanyika katika Hekalu Kaskazini Magharibi mwa China
Watu wa kabila la Wagelao washerehekea Sikukuu ya Maolong huko Guizhou, Kusini Magharibi mwa China
Wakulima kote China wawa na pilika nyingi za uzalishaji wa kilimo wakati Siku ya Yushui yakiwadia
Ndege C919 ya China yashiriki mazoezi ya Maonyesho ya Anga ya Singapore
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma