Lugha Nyingine
Uchumi wa Afrika Kusini wakadiriwa kukua kwa wastani wa asilimia 1.6 katika miaka 3 ijayo
Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Enoch Godongwana akitoa Hotuba ya Bajeti Mwaka 2024 mjini Cape Town, Afrika Kusini, Februari 21, 2024. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)
CAPE TOWN - Uchumi wa Afrika Kusini umekadiriwa kuwa ulikua kwa asilimia 0.6 mwaka jana na utaongezeka kwa wastani wa asilimia 1.6 katika miaka mitatu ijayo, Waziri wa Fedha Enoch Godongwana amesema Jumatano wakati akitoa Hotuba ya Bajeti Mwaka 2024 huko Cape Town, mji mkuu wa kibunge wa Afrika Kusini.
Godongwana amebainisha katika hotuba yake kuwa pamoja na kuimarika kwa mtazamo wa kimataifa wa mwaka 2024, ukuaji wa uchumi wa muda mfupi ujao wa Afrika Kusini unaendelea kutatizwa na bei ya chini ya bidhaa na vizuizi vya kimuundo.
“Tunakadiria ukuaji halisi wa Pato la Taifa kwa asilimia 0.6 Mwaka 2023. Hii ni chini kuliko asilimia 0.8 iliyokadiriwa wakati wa Taarifa ya Sera ya Bajeti ya Muda wa Kati ya Mwaka 2023,” amesema Godongwana.
Marekebisho hayo ya makadirio yametokana na matokeo hafifu kuliko ilivyotarajiwa katika robo ya tatu ya Mwaka 2023, hasa katika matumizi kwenye manunuzi ya kaya na uwekezaji wa mali zisizohamishika.
Pamoja na hayo, "kati ya Mwaka 2024 na 2026, ukuaji wa uchumi unatarajiwa kufikia wastani wa asilimia 1.6," Godongwana amesema. "Mtazamo wa ukuaji huo unaungwa mkono na kupunguzwa kwa hali ya upungufu wa umeme wakati ambapo miradi mipya ya nishati inapoanza uzalishaji, na huku mfumuko wa bei wa chini ukiunga mkono manunuzi ya kaya na upanuzi wa upatikanaji mkopo."
Waziri huyo wa fedha pia amesema nakisi ya bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 ilikadiriwa kuwa mbaya kwa kuchukua asilimia 4.9 ya Pato la Taifa kutoka asilimia 4 mwaka uliopita, ingawa amesema itaanza kuimarika kutoka mwaka 2024/2025 hadi kufikia wastani wa asilimia 4.5 ya Pato la Taifa na kufikia asilimia 3.3 ifikapo mwaka 2026/2027.
Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Enoch Godongwana akitoa Hotuba ya Bajeti Mwaka 2024 mjini Cape Town, Afrika Kusini, Februari 21, 2024. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)
Wakulima kote China wawa na pilika nyingi za uzalishaji wa kilimo wakati Siku ya Yushui yakiwadia
Ndege C919 ya China yashiriki mazoezi ya Maonyesho ya Anga ya Singapore
Chuo Kikuu cha Kenyatta chafanya maonyesho ya dragoni wa China ili kukuza mawasiliano ya kitamaduni
Mkoa wa Xizang, China wafungua maeneo ya utalii kwa umma bila tiketi ili kuhimiza utalii
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma