Lugha Nyingine
China yaanza sensa ya rasilimali za data
Mfanyakazi akitembea kuipita skrini kwenye Maabara Muhimu ya China ya Data Kubwa ya Umma katika Chuo Kikuu cha Guizhou huko Guiyang, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Mei 23, 2023. (Xinhua/Liu Xu)
Beijing – Idara ya Uhifadhi wa Data za kidijitali ya China imesema Jumatatu kuwa, China imeanzisha sensa ya kufanya tathmini na ufahamu wa uzalishaji, uhifadhi, mzunguko, biashara, utumiaji na usalama wa rasilimali za data kote nchini, ambapo sensa hiyo, inafanyika kuanzia Februari 18 hadi Machi 5, inalenga kutoa usaidizi wa kitakwimu kwa kutunga sera na kuanzishwa kwa miradi ya vielelezo ya majaribio.
Washiriki wa sensa hiyo ni pamoja na idara husika za serikali ngazi ya mikoa, watengenezaji wa vifaa vya kukusanya na kuhifadhi data, kampuni katika sekta za matumizi kwenye manunuzi na majukwaa ya intaneti za viwanda, kampuni za data kubwa na akili bandia, masoko ya rasilimali za data, na maabara ya kitaifa.
Sensa hiyo pia inahusisha viwanda vya kiserikali, mashirika ya shughuli mbalimbali, mashirikisho ya kibiashara, pamoja na Kituo cha Upashanaji Habari cha kitaifa vilivyosimamiwa na serikali kuu.
China ilianzisha kampeni ya miaka mitatu mwezi Disemba mwaka jana ya kuhimiza matumizi ya data kama kipengele cha uzalishaji katika hali zenye mahitaji makubwa, na kuahidi kuongeza juhudi za kuhamasisha na kuongeza matumizi ya data ya kiwango cha juu, kuhakikisha sifa bora ya utoaji wa data, kuboresha mazingira ya mzunguko wa data na kuimarisha usalama wa data.
Wakulima kote China wawa na pilika nyingi za uzalishaji wa kilimo wakati Siku ya Yushui yakiwadia
Ndege C919 ya China yashiriki mazoezi ya Maonyesho ya Anga ya Singapore
Chuo Kikuu cha Kenyatta chafanya maonyesho ya dragoni wa China ili kukuza mawasiliano ya kitamaduni
Mkoa wa Xizang, China wafungua maeneo ya utalii kwa umma bila tiketi ili kuhimiza utalii
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma