Lugha Nyingine
Rais Xi asema uhusiano kati ya China na Russia unakumbatia fursa mpya za maendeleo
Rais Xi Jinping wa China amesema China na Russia zimehimili mitihani mingi ya pamoja hapo awali, na kwamba uhusiano wa nchi hizo unakumbatia fursa mpya za maendeleo katika siku zijazo.
Rais Xi ameyasema hayo Tarehe 8, Februari katika mazungumzo yake ya simu na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin, kabla ya mwaka mpya wa jadi wa China ambapo pia walipeana salamu za mwaka mpya.
Akibainisha kuwa mwaka mpya wa jadi wa China umewadia , Rais Xi amesema watu wa China wamejaa matumaini na imani kuelekea Mwaka mpya wa Dragoni.
Akizungumzia kuhusu yeye na Putin kukutana mara mbili na kufikia makubaliano mengi muhimu katika mwaka uliopita, Rais Xi amesema chini ya mwongozo wa pamoja wa viongozi hao wawili, serikali, mabunge na vyama vya siasa vya nchi hizo mbili vimeshiriki katika mazungumzo ya dhati, na ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali umeonesha uthabiti na uhai.
Akibainisha kuwa mwaka huu ni mwaka wa 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia, Rais Xi amesema China iko tayari kuendelea kushikilia moyo wa kusaidiana na urafiki wa milele na Russia ili kuandika kwa pamoja ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Rais Putin amesema mwaka jana, ushirikiano kati ya Russia na China katika nyanja mbalimbali ulizaa matunda, na kueleza nia yake ya kuendelea kudumisha mawasiliano ya karibu na Rais Xi, ili viongozi hao wawili waweze kuziongoza nchi hizo mbili kufikia maendeleo mapya ya ushirikiano katika nyanja zote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma