Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa wajumbe wasio wanachama wa CPC
Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akishiriki katika mkutano wa kila mwaka wa kujumuika pamoja na wajumbe wasio wanachama wa CPC kabla ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Februari 7, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), Jumatano kwenye mkutano wa kila mwaka wa kujumuika pamoja na wajumbe wasio wanachama wa CPC katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing ametuma salamu za sikukuu kwa wajumbe hao wasio wanachama wa CPC na Shirikisho la Viwanda na Biashara la China (ACFIC), watu wasio na vyama, na watu wengine wa umoja wa mstari wa mbele kabla ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.
Rais Xi amesema, Mwaka 2023 ulikuwa mwaka usio wa kawaida. Katika mwaka mmoja uliopita, Kamati Kuu ya CPC ilikiongoza Chama kizima na wananchi wa China kutekeleza kikamilifu mipango na maagizo ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC na kufuata mwongozo wa kimsingi wa kutafuta maendeleo ya kazi kwa hatua madhubuti.
"Tumehimili shinikizo kutoka nje na kushinda matatizo ya ndani, tumefanya jitihada za pande zote ili kuimarisha uchumi na maendeleo, na tumefikia kwa mafanikio malengo makuu yaliyowekwa ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii," amesema Xi.
Tuna mwanzo mzuri wa kuanzia, na kuna mambo mengi muhimu katika jitihada zetu, Rais Xi amesema, huku akibainisha kuwa mafanikio mapya yamepatikana katika nyanja za uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia.
Kisha Rais Xi akatoa shukrani za dhati kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC.
Rais Xi amesema kuwa Mwaka 2024 ni maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, ni mwaka muhimu sana wa kutimiza malengo na majukumu yaliyoainishwa katika Mpango wa 14 wa Miaka Mitano wa nchi hiyo (2021-2025).
Rais Xi amesisitiza kuwa watu wa vyama mbalimbali vya kidemokrasia, na watu wasio na chama wanapaswa kusoma kwa kina ili kuelewa kikamilifu maamuzi na mipango mikuu ya Kamati Kuu ya CPC, na kuchangia hekima na nguvu zao katika kuendeleza maendeleo ya mambo ya kisasa ya China.
Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akishiriki katika mkutano wa kila mwaka wa kujumuika pamoja na wajumbe wasio wanachama wa CPC na kupiga picha ya pamoja kabla ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing mjini Beijing, China, Februari 7, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma