Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Geingob wa Namibia
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za rambirambi siku ya Jumatatu kwa Rais mpya wa Namibia aliyeapishwa Nangolo Mbumba kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Namibia Hage Geingob.
Rais Xi akiwa kwa niaba ya serikali ya China na watu wake, na kwa jina lake mwenyewe, ametoa salamu za dhati za rambirambi na kuonesha pole na masikitiko ya dhati kwa serikali ya Namibia na watu wake, pamoja na familia ya Geingob.
Katika ujumbe wake, Rais Xi ameeleza kwamba Rais Geingob, kiongozi bora wa Namibia, alihimiza maendeleo ya pande zote ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Namibia wakati wa uhai wake na kutoa mchango muhimu katika kukuza urafiki wa China na Namibia na Afrika.
Kifo chake ni hasara kubwa kwa watu wa Namibia, na watu wa China pia wamepoteza rafiki mzuri, Rais Xi amesema.
Ameongeza kuwa China inathamini urafiki wa jadi kati yake na Namibia na ingependa kushirikiana na upande wa Namibia katika kusukuma mbele maendeleo endelevu ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.?
Balozi: China imejikita katika kuendeleza uhusiano wa pande mbili na Ethiopia
Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China
Picha: Mandhari ya Ziwa Yundang la Xiamen, China katika ukungu
Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma