Lugha Nyingine
Chapa za Kimataifa zatilia maanani?soko la China kwa kuchangamkia fursa za "Mwaka?wa Dragoni"
Mapambo yenye kauli mbiu ya dragoni yakionekana katika picha kwenye Duka kubwa la Kimataifa la Mauazo ya Bidhaa bila Ushuru la Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Februari 1, 2024. (Xinhua/Guo Cheng)
HAIKOU – Wakati Mwaka Mpya wa Jadi wa China unapokaribia, chapa nyingi za kimataifa zimechangamkia fursa za utamaduni wa kalenda ya kilimo ya China na kuzindua bidhaa za toleo maalum la Mwaka wa Dragoni ili kukumbatia soko la China.
China itaingia katika Mwaka wa Dragoni Februari 10 kwa mujibu wa kalenda ya kilimo ya China.
Maduka makubwa ya bidhaa zisizotozwa ushuru katika mkoa wa Hainan, kusini mwa China yamepambwa kwa rangi nyekundu za sherehe na bidhaa zenye kauli mbiu ya dragoni. Chapa za kimataifa zinatoa bidhaa mbalimbali za Mwaka Mpya wa Jadi wa China, zikijumuisha vipodozi, nguo, mifuko, vito na vinywaji vikali, kwa njia ya kuvutia watumiaji wa China.
Miongoni mwa matoleo maalum ya Mwaka wa Dragoni ambayo yamechukua nafasi kubwa katika maduka yasiyotozwa ushuru ni seti onyeshi za Mwaka Mpya za Kampuni ya LEGO ziitawazo Auspicious Dragon, kitambaa cha Hariri chenye picha ya Dragoni cha Ferragamo na mkufu wa Chapa ya Swarovski wenye katuni ya dragoni, na kadhalika.
Mapambo yenye maudhui ya dragoni yakionekana katika picha kwenye Jengo la Maduka yasiyotozwa ushuru la Haikou Riyue huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Januari 27, 2024. (Xinhua/Guo Cheng)
Katika duka ya bidhaa zisizotozwa ushuru huko Haikou, mji mkuu wa Mkoa wa Hainan, mkazi wa eneo hilo aitwaye Tang Dan alikuwa akitazama bidhaa za kutunza ngozi kwenye kaunta ya Chapa ya Estée Lauder. Mara moja alivutiwa na seti mpya ya toleo maalum la Mwaka Mpya wa Jadi wa China.
"Kifungashio chekundu ni cha sherehe sana, na kina picha ya dragoni, inayowasilisha shamrashamra za Mwaka Mpya wa Jadi wa China," Tang amesema, huku akiongeza kuwa kati ya wanyama 12 wanaowakilisha miaka ya kalenda ya kilimo ya China, mnyama dragoni ni maalum zaidi, "Anaashiria siyo tu Taifa la China, lakini pia bahati nzuri."
Bidhaa za utunzaji wa ngozi za toleo maalumu la mwaka wa dragoni zikionekana katika picha kwenye jengo la maduka yasiyotozwa ushuru la Riyue huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Januari 27, 2024. (Xinhua/Guo Cheng)
Mavazi yenye picha ya dragoni yakionekana katika picha kwenye Jengo la maduka yasiyotozwa ushuru la Riyue huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Januari 27, 2024. (Xinhua/Guo Cheng)
Katika miaka ya hivi karibuni, chapa za kimataifa mara nyingi zimekuwa zikikumbatia vipengele vya utamaduni wa jadi wa China ili kutumia vizuri uwezo mkubwa wa soko kubwa la China.
Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China
Picha: Mandhari ya Ziwa Yundang la Xiamen, China katika ukungu
Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia
Mandhari ya kushangaza ya “Barabara Kuu inayoning’inia kwenye Miteremko ya Vilima” wakati wa theluji
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma