Lugha Nyingine
China yaendelea kuimarisha nafasi ya sekta ya mambo ya fedha katika kuhudumia uchumi halisi
Picha ya kumbukumbu ikionyesha mandhari ya nje ya Benki Kuu ya China mjini Beijing, China. (Xinhua/Peng Ziyang)
BEIJING - China inaendelea kufanya juhudi madhubuti kuongeza mchango wa sekta ya mambo ya fedha katika kuhudumia uchumi halisi kama lengo la msingi la maendeleo yenye ubora wa juu ya mambo ya fedha, wataalam na wadao wa sekta hiyo wamesema.
“Tangu mwaka jana taasisi za fedha zimeendelea kuimarisha ugawaji wa rasilimali katika maeneo muhimu na viungo hafifu kama vile uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, miundombinu, biashara ndogo na za kati za kibinafsi na maendeleo ya kijani, na zimeonyesha sifa za wazi za kutumikia maendeleo yenye ubora wa juu," amesema Dong Ximiao, mtafiti mkuu katika Kampuni ya Watumiaji wa Mambo ya Fedha ya Merchants Union.
Haya ni maendeleo mapya yanayoangazia ahadi zilizotolewa katika mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuhusu kazi ya mambo ya fedha uliofanyika Beijing mwishoni mwa Oktoba mwaka jana. Mkutano huo ulibainisha kuwa rasilimali zaidi za kifedha zinapaswa kutumiwa katika kusaidia uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, viwanda vya teknolojia ya hali ya juu, maendeleo ya kijani, biashara ndogo na za kati, pamoja na mikakati ya maendeleo yanayoendeshwa na uvumbuzi na mikakati iliyoratibiwa ya maendeleo ya eneo husika.
Sera hizi zinapoanza kutumika, kampuni nyingi zilitiwa nguvu. Mwanzoni mwa mwaka huu mpya, Yan Bing, meneja wa wateja wa Benki ya Everbright ya China Tawi la Nanjing, ametembelea kampuni 12 bila kukoma na kutoa mikopo ya yuan karibu milioni 200 (kama dola milioni 28.15 za Marekani).
"Mwaka jana, Benki ya Everbright ya China iliuchukua 'Ufadhili wa kifedha katika sekta ya Sayansi na teknolojia' kama mojawapo ya njia tatu za kuendeleza biashara yetu," amesema Yan.
Benki na taasisi nyingine za kifedha nchini China kama vile Benki ya Viwanda na Biashara ya China (ICBC) pia zinagombea fursa zinazoibuka katika kuhudumia uchumi halisi.
Li Duo, mkuu wa idara ya usimamizi wa mikopo na uwekezaji ya ICBC, amesema kuwa ICBC inaunga mkono kwa kiasi kikubwa sekta zikiwemo nishati safi, usafirishaji usiochafua mazingira, uhifadhi wa nishati na ulinzi wa mazingira.
Mwaka 2023, mikopo ya China ya yuan iliyotolewa kwa uchumi halisi iliongezeka kwa asilimia 10.4 hadi kufikia Yuan trilioni 235.48, ikichukua asilimia 62.3 ya jumla ya ufadhili wa kifedha wa Yuan trilioni 378.09.
Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China
Picha: Mandhari ya Ziwa Yundang la Xiamen, China katika ukungu
Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia
Mandhari ya kushangaza ya “Barabara Kuu inayoning’inia kwenye Miteremko ya Vilima” wakati wa theluji
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma