Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping asisitiza kuendeleza nguvu za uzalishaji zenye sifa mpya na maendeleo yenye sifa bora
BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), Jumatano alipokuwa akiongoza semina elelezi ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC amehimiza kuharakisha kuendeleza nguvu za uzalishaji zenye sifa mpya na kusukuma mbele kithabiti maendeleo yenye sifa bora, huku akisisitiza kuwa maendeleo yenye sifa bora ni kanuni isiyobadilika katika Zama Mpya.
"Kuendeleza nguvu za uzalishaji zenye sifa mpya ni mahitaji ya kimsingi na lengo muhimu la kuhimiza maendeleo yenye sifa bora, na ni muhimu kuendelea kutumia kikamilifu uvumbuzi ili kuharakisha kuendeleza nguvu za uzalishaji zenye sifa mpya," Rais Xi amesema.
Rais Xi amedhihirisha, kwamba kuhimiza maendeleo yenye sifa bora kumekuwa maoni ya kauli moja na vitendo vya hiari vya Chama kizima na jamii nzima katika zama mpya, lakini bado kuna sababu nyingi zinazozuia maendeleo hayo, na ni lazima yaongozwe kwa nadharia mpya kuhusu nguvu za uzalishaji zenye sifa mpya
Huku uvumbuzi ukichukua jukumu kuu, nguvu za uzalishaji zenye sifa mpya zinamaanisha kuondokana na njia ya kijadi ya ukuaji wa uchumi na njia ya kijadi ya maendeleo ya tija, na zitakuwa nguvu za uzalishaji za kiwango cha kimaendeleo zenye umaalum wa teknolojia ya hali ya juu, ufanisi mkubwa na sifa bora, ambazo zinaendana na dhana mpya kuhusu maendeleo.
Amesema, nguvu za uzalishaji zenye sifa mpya zinapatikana kutokana na mafanikio ya kiteknolojia ya kimapinduzi, upangaji bunifu wa mambo ya uzalishaji, na viwanda vinavyobadilishwa miundo na kupandishwa ngazi ya maendeleo; msingi wake ni kupandishwa ngazi na kuboreshwa kwa uundaji wa wafanyakazi, raslimali za uzalishaji na nguvukazi, na alama ya kiini chake ni kuinuliwa juu kwa kiasi kikubwa tija ya uzalishaji kutokana na vipengele vyote, umaalumu wake ni uvumbuzi, umuhimu wake ni sifa bora, na hali yake ni nguvu za uzalishaji za kiwango cha kimaendeleo.
Rais Xi ameeleza kuwa, ni lazima kuimarisha uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, hasa uvumbuzi wenye hakimiliki na unaoleta mambo mapya, kuharakisha kutimiza lengo la kujitegemea na kuwa na nguvu kubwa na kiwango cha juu katika sayansi na teknolojia, na kupigania kwa bidii mafanikio ya teknolojia ya msingi na muhimu, ili matokeo ya uvumbuzi wenye hakimiliki na unaoleta mambo mapya wa kisayansi na kiteknolojia yatapatikana mfululizo, na kuwa uwezo na msukumo wa kuendeleza nguvu za uzalishaji zenye sifa mpya.
Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China
Picha: Mandhari ya Ziwa Yundang la Xiamen, China katika ukungu
Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia
Mandhari ya kushangaza ya “Barabara Kuu inayoning’inia kwenye Miteremko ya Vilima” wakati wa theluji
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma