Lugha Nyingine
Vitu vya kuleta Baraka na Bahati ya Kimali vyauzwa vizuri kwenye maduka nchini China
Picha hii iliyopigwa Januari 10, 2024 ikionyesha vibandiko vya jokofu vyenye picha za dragoni kwenye duka la bidhaa maalum mjini Beijing, China. Chapa kuu nchini China zimetoa bidhaa za kitamaduni zenye umaalum wa mwaka wa dragoni wa jadi wa China unaokaribia kuwadia. (Xinhuanet/Liu He)
Mwaka Mpya wa Jadi wa China unapokaribia, wanunuzi vijana wa China wameanza kununua bidhaa zinazoashiria Baraka ili kukidhi mahitaji ya kihisia na kupata bahati ya kimali, mawimbi hayo ya ununuzi yamechochea ukuaji wa biashara kwa watengenezaji wa bidhaa hizo ndogo ndogo ambapo bidhaa hizo zikiwemo vibandiko vya jokofu vyenye picha za Mungu wa utajiri, na vifuniko vya simu za mkononi vyenye maandiko ya Kichina ya kutakia heri na Baraka zinauzwa kwa wingi.
Mwezi Januari, kiasi cha mauzo ya bidhaa ndogo ndogo zenye picha za Mungu wa utajiri kiliongezeka mara sita kuliko mwaka uliopita kwenye Karakana ya Tao, jukwaa la biashara mtandaoni la Taobao ambalo hutoa bidhaa moja kwa moja kutoka kwa viwanda vinavyozitengeneza.
Kwa vifuniko vya simu za mkononi, vijana wanapendelea mitindo iliyochapishwa kwa maneno au mwelekeo unaoashiria hisia au matarajio yao ya kipekee.
Bidhaa kama vile bahasha nyekundu zilizoundwa kwa ajili ya Mwaka mpya wa Dragoni wa jadi wa China pia zimekuwa maarufu, na mauzo yake yamezidi yale ya bahasha nyekundu katika Mwaka wa Sungura utakaopita siku chache baadaye, Karakana ya Tao imesema.
Vijana wa China wanatilia maanani zaidi Mungu wa utajiri, Baraka na bahati ya kimali, na hii imechochea matumizi katika manunuzi ya bidhaa zinazowafurahisha.
Jessica Liu, mfanyakazi wa ofisini mwenye umri wa miaka 30 mjini Beijing, amesema hivi majuzi alitumia yuan 2,000 hivi (kama dola 279 za Kimarekani) kwa kununua sanamu ya jade ya Mungu wa mali.
Anaamini kuwa sanamu hiyo imempa faraja ya kisaikolojia na kumsaidia kupata pesa zaidi.
"Uchumi wa kihisia ni sehemu muhimu ya ukuaji wa uchumi katika zama za kidijitali. Dhana hiyo ilitokana na maendeleo ya kiteknolojia na mahitaji ya kisaikolojia ya watu, ambayo imeleta fursa zaidi za biashara kwa wafanyabiashara," Hong Yong, mtafiti wa Idara ya utafiti wa biashara ya mtandaoni katika Taasisi ya Biashara, Uchumi na Ushirikiano ya Kimataifa ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma