Lugha Nyingine
Mji wa Beijing, China washuhudia?ukuaji wa utalii wa barafu na theluji
Watalii wakiendesha baiskeli ambazo zimeunganishwa na vifaa vya kuteleza kwenye barafu katika Kasri la Kale la Kifalme (Summer Palace) mjini Beijing, China, Januari 1, 2024. (Xinhua/Chen Yehua)
BEIJING - Wakati wa majira ya baridi, Ziwa Kunming la Kasri la Kale la Kifalme (Summer Palace), eneo lililoorodheshwa na UNESCO kuwa Urithi wa Dunia mjini Beijing, ambalo ni uwanja wa asili wa kuteleza kwenye barafu katika sehemu ya Kaskazini-Magharibi ya Beijing wenye eneo lenye ukubwa wa jumla ya mita za mraba 350,000, ambalo linaweza kupokea watu 5,000 kwa wakati mmoja, kwa kawaida huwa uwanja mkuu wa kuteleza kwenye barafu wa Beijing katika majira ya baridi.
Mwezi Januari mwaka huu, lilipokea watu zaidi ya 230,000 katika shughuli kama vile mbio za mikokoteni za kwenye barafu na kuteleza kwa kasi kwenye barafu.
Raundi kadhaa za theluji iliyoanguka msimu huu wa baridi imepamba majengo ya kale katika bustani hiyo, na kuvutia watalii wengi.
"Kuteleza kwenye ziwa la barafu katika bustani ya kale ya kifalme, mbele ya madaraja maarufu yenye umbo la upinde, ni kama ndoto kwangu," amesema mtalii mwenye jina la ukoo la Liu kutoka Shanghai.
Baada ya kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Mwaka 2022, Beijing imekuwa na maeneo mengi ya michezo hiyo kwa mashindano ya kimataifa ya michezo ya majira ya baridi katika msimu huu wa baridi.
Bustani ya Shougang ya Beijing, eneo maarufu wakati wa Michezo hiyo, imekaribisha kurejea kwa michezo ya kuruka angani na kuteleza kwenye barafu kwa michezo ya FIS Snowboard na Kombe la Dunia la Freeski Big Air kati ya Novemba 30 na Desemba 2 Mwaka 2023.
Maeneo zaidi ya 10 ya kibiashara katika mji mkuu huo wa China yametoa kumbi zaidi ya 100 za barafu na theluji, zikiandaa mfululizo wa shughuli za burudani. Ofisi ya michezo ya Beijing pia imeandaa shughuli 15 za michezo ya umma, na kuhimiza wakazi wa eneo hilo kupata uzoefu wa michezo ya barafu na theluji.
Kwa sasa Beijing inajivunia eneo lenye ukubwa wa mita za mraba zaidi ya milioni 1 la viwanja vya barafu na maeneo ya kuteleza kwenye theluji. Ofisi ya utamaduni na utalii ya Beijing imeteua shughuli za barafu na theluji kuwa sehemu mpya ya ukuaji kwa maendeleo ya utalii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma