Lugha Nyingine
Xi Jinping aongoza mkutano wa viongozi wa CPC kupitia ripoti, kanuni
BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), aliongoza mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC siku ya Jumatano ambao umepitia ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC.
Kazi hiyo ya mapitio imefanyika baada ya mkutano huo kusikiliza na kujadili ripoti za kazi za vikundi vya uongozi wa Chama vya Bunge la Umma la China, Baraza la Serikali la China, Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), Mahakama Kuu ya Umma ya China (SPC), na Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China (SPP), pamoja na ripoti ya kazi ya Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC.
Mambo mengine yaliyopitiwa pia katika mkutano huo ni ripoti ya majumuisho kuhusu programu ya kusoma kinadharia Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China kwa Zama Mpya, mwongozo wa kuimarisha mafanikio katika programu hiyo ya kusoma kinadharia, na kanuni za CPC kuhusu ukaguzi wa nidhamu.
Wahudhuriaji wa mkutano huo wametambua kikamilifu kazi ya vikundi vya uongozi wa chama katika vyombo hivyo vilivyotajwa pamoja na kazi ya Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, na wameidhinisha mipango yao ya kazi ya Mwaka 2024.
Mkutano huo umehimiza juhudi endelevu za kuhakikisha utekelezaji wa maamuzi ya kimkakati yaliyotolewa katika Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC huku kukiwa na kujikita katika kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.
Mkutano huo umesisitiza kuchukulia kazi ya kupata maendeleo ya kiwango cha juu kuwa kazi kuu ya kwanza ya Mwaka 2024, kufanya juhudi za kuongeza kihalisi sifa bora ya maendeleo ya uchumi na mafanikio hitajika kwa wingi katika mambo ya uchumi. Pia umesisitiza kuboresha maisha ya watu na kulinda usawa na haki kwenye jamii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma