Lugha Nyingine
IMF yaongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi duniani Mwaka 2024 hadi asilimia 3.1
Watu wakitembea kuyapita makao makuu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Washington, D.C., Marekani, Aprili 10, 2023.(Xinhua/Liu Jie)
WASHINGTON - Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Jumanne limeongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi duniani hadi asilimia 3.1 kwa Mwaka 2024, ikiwa ni asilimia 0.2 zaidi ya Oktoba mwaka jana, kwa mujibu wa taarifa yake mpya ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia (WEO) ambapo imesema makadirio hayo ya juu yanaakisi kuongezeka kwa makadirio ya uchumi wa China, Marekani, na masoko makubwa yanayoibukia na nchi zinazoendelea kiuchumi.
Hata hivyo, makadirio ya ukuaji wa uchumi duniani katika Mwaka 2024 na 2025 ni ya chini ya ukuaji wa wastani wa kihistoria wa asilimia 3.8 katika Mwaka 2000-2019, ikionyesha sera za kifedha zenye vizuizi na kuondolewa kwa uungaji mkono wa kifedha, pamoja na ukuaji mdogo wa uzalishaji, IMF imesema.
"Uchumi wa kimataifa unaendelea kuonyesha hali ya ajabu ya unyumbufu ya uchumi, huku mfumuko wa bei ukipungua kwa madhubuti na ukuaji wa uchumi ukidumisha kasi yake, uwezekano wa ongezeko la uchumi umeongezeka, lakini kasi ya upanuzi bado ni ndogo," Mchumi Mkuu wa IMF Pierre-Olivier Gourinchas amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari huko mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Ukuaji wa uchumi nchini China unakadiriwa kuwa asilimia 4.6 Mwaka 2024, ukiwa na marekebisho ya juu ya asilimia 0.4 tangu WEO mwezi Oktoba. Kwa Marekani, ukuaji unakadiriwa kuwa asilimia 2.1 Mwaka 2024, asilimia 0.6 zaidi ya makadirio ya Oktoba. Kwa Eneo la Euro, ukuaji unakadiriwa kuwa asilimia 0.9 Mwaka 2024, asilimia 0.3 chini ya makadirio ya awali.
IMF imebainisha kuwa mfumuko wa bei unashuka kwa kasi zaidi kuliko ilivyotarajiwa katika kanda nyingi, huku kukiwa na masuala ya upande wa utoaji na vizuizi vya sera ya fedha.
Gourinchas, hata hivyo, ameonya kuwa msukosuko mpya wa siasa za kijiografia, hasa katika Mashariki ya Kati na kuongezeka kwa mashambulio dhidi ya meli katika Bahari Nyekundu, kunaweza kuvuruga minyororo ya bidhaa kuu na usambazaji, ambayo inaweza kuchochea mfumuko wa bei wa kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma