Lugha Nyingine
Mikataba ya ushirikiano yenye thamani ya Yuan bilioni 13.6?yasainiwa kwenye Maonyesho ya biashara kati ya China na Russia
Washiriki wakihudhuria mkutano wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Russia uliofanyika Shenyang, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China, Januari 29, 2024. (Xinhua/Yang Qing)
SHENYANG – Mikataba jumla ya 55, kwa pamoja ikiwa na thamani ya yuan bilioni 13.6 (dola bilioni 1.91 za Kimarekani), imetiwa saini siku ya Jumatatu na kampuni za China na washirika wao wa kibiashara wa Russia huko Shenyang, Mji Mkuu wa Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China.
Mikataba hiyo inahusu sekta kama vile ghala la mnyororo wa bidhaa baridi, huduma za mambo ya fedha, na uagizaji na uuzaji nje wa bidhaa, ambayo imetiwa saini katika mkutano wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Russia uliofanyika Shenyang.
Wajasiriamali zaidi ya 100 kutoka Russia na nchi nyingine wa Umoja wa Kiuchumi wa Eurasia wameshiriki kwenye shughuli hiyo, pamoja na wawakilishi wa kampuni za China, wataalam wa viwanda na wasomi.
Serikali ya mji wa Shenyang na Idara ya Biashara ya Mkoa wa Liaoning ni miongoni mwa waandaaji wa shughuli hiyo.
Serikali ya mji wa Shenyang na Shirika la Ndege la China Eastern zimetia saini waraka wa kuonyesha nia katika mkutano huo, zikikubaliana kufungua njia ya kawaida ya ndege za abiria kati ya Shenyang na Moscow mwishoni mwa Februari.
Washiriki wakihudhuria mkutano wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Russia uliofanyika Shenyang, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China, Januari 29, 2024. (Xinhua/Yang Qing)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma