Lugha Nyingine
Rais Xi atoa hotuba ya video kwenye mapokezi ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ufaransa
Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba ya video kwenye mapokezi ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ufaransa mjini Beijing, China, Januari 25, 2024. (Xinhua/Li Xueren)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametoa hotuba kwa njia ya video siku ya Alhamisi mjini Beijing kwenye mapokezi ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ufaransa akisema kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ufaransa miaka 60 iliyopita lilikuwa tukio kubwa katika historia ya uhusiano wa kimataifa.
Kwa hekima na ujasiri wao, Mwenyekiti Mao Zedong na Jenerali Charles de Gaulle walifungua mlango wa mawasiliano na ushirikiano kati ya China na nchi za Magharibi, na kuleta matumaini kwa Dunia wakati wa Vita Baridi, Rais Xi ameeleza.
Amesema katika miaka 60 iliyopita, uhusiano kati ya China na Ufaransa siku zote umekuwa mstari wa mbele katika uhusiano wa China na nchi za Magharibi, ukileta manufaa kwa watu wa pande hizo mbili na kuchangia amani, utulivu na maendeleo ya Dunia.
Historia ya kipekee ya uhusiano kati ya China na Ufaransa imeundwa kwa "moyo wa China na Ufaransa" ulio wa kujitegemea, kuelewana, muono wa mbele, ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja, Rais Xi amesisitiza huku akiongeza kuwa, katika kukabiliana na changamoto za zama mpya, China na Ufaransa zinapaswa kushikilia nia ya awali ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, kutupia macho siku za baadaye, na kuthubutu kufanya juhudi kubwa ili kupata maendeleo makubwa zaidi.
Ametoa wito kwa pande hizo mbili kutetea kwa pamoja Dunia ya ncha nyingi yenye usawa na utaratibu na utandawazi wa kiuchumi ambao ni jumuishi na wenye manufaa kwa wote, na kuendelea kuchangia katika kudumisha amani na utulivu duniani na kutatua changamoto za kimataifa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia ametoa hotuba kwa njia ya video.
Macron amesema miaka 60 iliyopita, Jenerali Charles de Gaulle alitazama kwa kupindua kiasi cha mantiki ya mapambano ya kambi na kufanya uamuzi wa kihistoria wa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Watu wa China.
Amesema, leo pande hizo mbili zina wajibu wa kuendeleza malengo makubwa yaliyowekwa Mwaka 1964 na kuendelea kushirikiana ili kujenga uhusiano wa wenzi ambao siyo tu unakidhi mahitaji ya mataifa hayo mawili, bali pia unachangia amani na utulivu duniani.
Bidhaa zenye umbo la Dragoni zapendwa kwenye maduka nchini China
Ndege mtilili mwenye koo nyeupe aonekana katika bustani ya Mji wa Xiamen, Kusini Mashariki mwa China
Katika Picha: Maonyesho ya taa za kijadi ya bustani ya Yuyuan mjini Shanghai, China
Watu washerehekea Sikukuu ya Timket huko Addis Ababa, Ethiopia
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma