Lugha Nyingine
China yachukua hatua kutuliza soko la mitaji, kuboresha imani
Picha ya kumbukumbu ikionyesha mandhari ya nje ya Soko la Hisa la Shanghai katika Eneo Jipya la Pudong mjini Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua)
Beijing - China imetuma ishara wazi kwamba juhudi zaidi zitafanywa ili kuleta utulivu kwenye soko la mitaji na kuboresha imani ya wawekezaji ambapo watunga sera wa nchi hiyo wamearifiwa juu ya uendeshaji wa soko la mitaji na mambo ya kuzingatia katika mkutano wa Baraza la Serikali la China uliofanyika siku ya Jumatatu.
China itaboresha zaidi utaratibu wa msingi wa soko la mitaji, kutilia maanani zaidi kudumisha uwiano thabiti kati ya uwekezaji na mambo ya fedha, kuongeza ubora na thamani ya uwekezaji wa makampuni zilizoorodheshwa kwenye soko la mitaji, kuongeza mtiririko wa fedha za muda wa kati na wa mrefu katika soko, na kuimarisha utulivu wa asili wa soko, kwa mujibu wa mkutano huo.
Mkutano huo unaonyesha umuhimu mkubwa ambao mamlaka inaweka katika maendeleo ya soko la mitaji na wasiwasi wa wawekezaji, amesema Peng Wensheng, mchambuzi mkuu wa Shirika la Mitaji la Kimataifa la China.
Zhang Wangjun, Afisa wa Kamati ya Udhibiti wa Dhamana ya China (CSRC), amesema mengi zaidi yatafanywa kuufanyia mageuzi katika uwekezaji wa soko la mitaji, kuhimiza uwekezaji wa taasisi wakati wa gharama nafuu, na kuboresha njia za uwekezaji za mifuko ya hifadhi ya jamii, mifuko ya bima na mifuko ya fedha za kila mwaka za kampuni kwa nia ya kukuza nguvu za muda mrefu za uwekezaji.
CSRC itaboresha tathmini ya ubora na usimamizi ulioainishwa wa kampuni zilizoorodheshwa kwenye soko la mtaji, na kuzielekeza katika kunufaisha zaidi wawekezaji kupitia ununuzi wa hisa na kughairi, na kuongeza gawio, amesema.
Uwiano wa fedha za muda wa kati na wa mrefu unaendelea kuwa chini katika soko la mitaji la China, na uungaji mkono zaidi wa sera unapaswa kuanzishwa ili kuhimiza fedha hizo kuingia sokoni, amesema Li Xunlei, mwanauchumi mkuu wa kampuni ya Dhamana ya Zhongtai.
Mkutano huo umeahidi kuchukua hatua imara na madhubuti zaidi za kuleta utulivu katika soko na kuboresha imani.
Katika Picha: Maonyesho ya taa za kijadi ya bustani ya Yuyuan mjini Shanghai, China
Watu washerehekea Sikukuu ya Timket huko Addis Ababa, Ethiopia
Sehemu ya pili ya mradi wa jengo la Kituo cha Mambo ya Fedha cha Nanjing wawekewa vifuniko
Umoja wa Mataifa kuchapisha stempu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa 2024
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma