Lugha Nyingine
Uchumi wa dijitali wachangia asilimia 42 katika Pato la Mkoa wa Guizhou wa China
Mfanyakazi akitambulisha mfumo wa usafiri unaotumia teknolojia ya data kubwa katika kituo cha data cha Kampuni ya China Mobile, kilichoko Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Mei 24, 2022. (Xinhua/Ou Dongqu)
GUIYANG - Uchumi wa dijitali ulichangia asilimia 42 ya thamani ya jumla ya uzalishaji (GDP) ya Mkoa wa Guizhou, Kusini Magharibi mwa China Mwaka 2023 ambapo takwimu kutoka kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu zinaonyesha kuwa GDP ya mkoa huo ilipita yuan trilioni 2.09 (kama dola bilioni 291 za Kimarekani) Mwaka 2023, ikirekodi ongezeko la asilimia 4.9 kuliko mwaka uliopita.
Peng Xianhua, Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya mkoa huo, amesema kuwa Guizhou imeshuhudia ongezeko kubwa katika nguvu zake za mifumo ya kompyuta mwaka jana kama moja ya vituo vinane vya kitaifa vya kompyuta vilivyoteuliwa na China, huku kukiwa na chip za kompyuta zaidi ya 70,000 zinazotumika sasa katika mkoa huo, sawa na ongezeko la mara 93 la mwaka hadi mwaka.
Guizhou pia imefikia hatua kubwa na muhimu zaidi katika ujenzi wa miundombinu ya teknolojia ya 5G, ikianzisha vituo 35,000 katika maeneo muhimu, maeneo maalum ya viwanda na vituo vya usafiri mwaka jana.
Tangu mkoa huo ulipoidhinishwa kujenga eneo la kwanza la kitaifa la majaribio la data kubwa Mwaka 2016, umekuwa mstari wa mbele katika tasnia ya data kubwa ya China.
Watu washerehekea Sikukuu ya Timket huko Addis Ababa, Ethiopia
Sehemu ya pili ya mradi wa jengo la Kituo cha Mambo ya Fedha cha Nanjing wawekewa vifuniko
Umoja wa Mataifa kuchapisha stempu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa 2024
Watu wa sehemu mbalimbali za China wajiandaa kwa Mwaka Mpya kwa kalenda ya jadi ya China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma