Lugha Nyingine
China yahimiza sekta mpya zenye nguvu ya ushindani ili kuimarisha biashara ya nje Mwaka 2024
Meli ya kusafirisha magari ya "BYD EXPLORER NO." ikiwasili kwenye Bandari ya Kimataifa ya Usafirishaji ya Xiaomo mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Januari 14, 2024. (Xinhua)
BEIJING – China inahimiza kwa juhudi kubwa sekta mpya zenye nguvu ya ushindani kutoka kwenye magari yanayotumia umeme hadi majukwaa ya biashara ya mtandaoni ili kutuliza biashara ya nje mwaka huu dhidi ya hali ya uchumi wa kimataifa uliodorora.
Meli ya kusafirisha mizigo ya "ro-ro" (roll-on/roll-off) iliyobeba magari zaidi ya 5,000 yanayotumia nishati mpya ilianza safari yake ya kwanza wiki iliyopita kutoka Bandari ya Shenzhen katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. Meli hiyo iliyokodishwa kwa kampuni ya kutengeneza magari ya BYD ya China imesafiri kuelekea bandari za Vlissingen nchini Uholanzi na Bremerhaven nchini Ujerumani.
Biashara ya uuzaji wa magari nje iliibuka kuwa moja ya sekta zilizofanya vizuri katika biashara ya nje ya China. Huku magari milioni 4.91 yakisafirishwa nje ya nchi Mwaka 2023, nchi hiyo inatarajiwa kuwa nchi inayouza magari mengi zaidi nje duniani.
Nguo, samani na vifaa vya nyumbani – ambazo zilikuwa ni bidhaa kuu kutoka China siku za nyuma –zimechukuliwa na "aina tatu mpya za bidhaa" za magari ya abiria yanayotumia umeme, betri za nishati ya jua na betri za lithiamu-ion, ambazo kwa pamoja zimerekodi mauzo ya nje yenye thamani ya yuan zaidi ya trilioni 1 (kama dola bilioni 140 za Kimarekani) mwaka jana.
"Uvumbuzi ni muhimu hasa katika soko la kimataifa lililojaa bidhaa," amesema Zhang Wei, Naibu Mkuu wa Akademia ya Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kiuchumi ya China chini ya Wizara ya Biashara, alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu mabadiliko ya muundo wa mauzo ya nje ya China.
Kampuni za kibiashara za China hazitegemei tena bei ya chini tu bali zinajivunia faida mpya za teknolojia ya hali ya juu, thamani ya juu iliyoongezwa, na ubora wa juu wa bidhaa, Fang Xueyu, mkuu wa kitengo cha masoko ya kimataifa wa Kampuni ya Hisense, amesema.
Ukiacha bidhaa za kiteknolojia, majukwaa yanayoshamiri ya biashara ya mtandaoni pia yametoa msukumo kwa biashara ya nje ya China.
"Kampuni nyingi ambazo zilikuwa zikijishughulisha na biashara ya ndani pekee wanaenda ng'ambo kwa njia hii," Guo amesema.
Mwaka 2023, thamani ya uagizaji na uuzaji nje wa bidhaa za kielektroniki wa kuvuka mipaka wa China ilifikia yuan trilioni 2.38, ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.6 kutoka mwaka mmoja uliopita.
Mustakabali wa biashara ya China kwa mwaka huu pia utakuwa mzuri, kutokana na dhamira isiyoyumba ya kufungua mlango.
Licha ya biashara kimataifa inayodidimia, China imefungua mlango wake wazi zaidi kwa Dunia, huku kukiwa na juhudi za kuhimiza ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuboresha maeneo yake ya majaribio ya biashara huria, na kupanua mtandao wa makubaliano ya biashara huria (FTAs) na nchi nyingine.
Watu washerehekea Sikukuu ya Timket huko Addis Ababa, Ethiopia
Sehemu ya pili ya mradi wa jengo la Kituo cha Mambo ya Fedha cha Nanjing wawekewa vifuniko
Umoja wa Mataifa kuchapisha stempu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa 2024
Watu wa sehemu mbalimbali za China wajiandaa kwa Mwaka Mpya kwa kalenda ya jadi ya China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma