Lugha Nyingine
China yatoa mpango wa majaribio ya mageuzi ya pande zote ya Eneo Jipya la Pudong
Picha ya kumbukumbu ikionyesha mwonekano wa nje wa Soko la Hisa la Shanghai katika Eneo Jipya la Pudong la Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua)
BEIJING - Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Ofisi Kuu ya Baraza la Serikali la China zimetoa mpango wa utekelezaji wa majaribio ya mageuzi ya pande zote ya Eneo Jipya la Pudong la Shanghai, Mashariki mwa China.
Mpango huo, uliopangwa kutekelezwa katika kipindi cha Mwaka 2023-2027, unalenga kuunga mkono mageuzi na ufunguaji mlango wa kiwango cha juu wa Eneo Jipya la Pudong, pamoja na kufanya juhudi za kulijenga Pudong kuwa eneo linaloongoza kwa maendelo ya mambo ya kisasa ya kijamaa.
Kwa mujibu wa mpango huo, Eneo Jipya la Pudong litapewa haki kubwa zaidi ya kujiamulia katika mageuzi kwenye "maeneo muhimu" na "viunganishi muhimu".
Mpango huo unaunga mkono eneo jipya hilo liwe mtangulizi wa kukamilisha mifumo na taratibu katika nyanja zote, kuharakisha ujenzi wa mfumo wa uchumi wa soko huria la kijamaa la kiwango cha juu, na kuboresha mfumo wa usimamizi na uwezo wa usimamizi, ili eneo jipya hilo lifanye kazi ya kuongoza katika juhudi za za kujenga nchi ya mambo ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa yenye umaalum wa China.
Watu washerehekea Sikukuu ya Timket huko Addis Ababa, Ethiopia
Sehemu ya pili ya mradi wa jengo la Kituo cha Mambo ya Fedha cha Nanjing wawekewa vifuniko
Umoja wa Mataifa kuchapisha stempu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa 2024
Watu wa sehemu mbalimbali za China wajiandaa kwa Mwaka Mpya kwa kalenda ya jadi ya China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma