Lugha Nyingine
Mauzo ya bidhaa zisizotozwa ushuru yaongeza biashara ya nje ya Mji wa Sanya wa China
Watalii wakitembelea jengo la maduka mengi yanayouza bidhaa zisizotozwa ushuru mjini Sanya, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Septemba 30, 2023. (Xinhua/Guo Cheng)
HAIKOU - Forodha ya Sanya siku ya Jumapili ilisema kuwa, uagizaji bidhaa na uuzaji bidhaa nje katika mji huo wa mapumziko wa Sanya nchini China uliongezeka na kufikia yuan bilioni 24.23 (kama dola za kimarekani bilioni 3.4) Mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 13.1 kuliko mwaka 2022, huku mauzo ya bidhaa zisizotozwa ushuru yakitoa mchango muhimu.
Mwaka 2023, katika mji wa Sanya wa Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, uagizaji wa bidhaa zisizotozwa ushuru kutoka nje ulipata ongezeko la asilimia 25.5, thamani yake ya jumla ilifikia yuan bilioni 10.76 ambayo ilichukua asilimia 44.4 ya thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji nje bidhaa wa mji huo.
Kampuni za biashara za kibinafsi zilipata ukuaji wa mara 1.8 katika uagizaji bidhaa na uuzaji bidhaa nje wakati kampuni za biashara zilizowekezwa na mtaji kutoka nje ziliongezeka mara 1.1.
Umoja wa Ulaya, Uswisi na Japan ziliibuka kuwa washirika wakuu watatu wa Mji wa Sanya katika biashara.
Vipodozi vya urembo na vitu vinavyotumika maliwatoni ni bidhaa kuu zilizoagizwa kwa wingi kutoka nje. Sanya iliagiza kutoka nje vipodozi vya urembo na vitu vya kutumika maliwatoni vyenye thamani ya yuan bilioni 5.67 Mwaka 2023, ikichukua asilimia 27.2 ya jumla ya bidhaa zote za mji huo katika kipindi hicho.
Sehemu ya pili ya mradi wa jengo la Kituo cha Mambo ya Fedha cha Nanjing wawekewa vifuniko
Umoja wa Mataifa kuchapisha stempu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa 2024
Watu wa sehemu mbalimbali za China wajiandaa kwa Mwaka Mpya kwa kalenda ya jadi ya China
Pilikapilika za uvuvi wa majira ya baridi katika Mkoa wa Hunan, Katikati ya China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma