Lugha Nyingine
Mji?wa Beijing, China watangaza malengo ya kiuchumi kwa Mwaka 2024
Magari yakiendeshwa kwenye Eneo Kuu la Kibiashara (CBD) katika Eneo la Chaoyang mjini Beijing, China, Juni 6, 2022. (Xinhua/Ju Huanzong)
BEIJING - Kufuatia mwaka wenye matunda ya mafanikio katika nyanja nyingi, Manispaa ya Beijing nchini China imeweka malengo ya kiuchumi kwa Mwaka 2024, ikilenga ukuaji wa uchumi wa mwaka hadi mwaka wa takriban asilimia 5 katika pato la taifa (GDP), kwa mujibu wa Meya wa Mji wa Beijing, Yin Yong.
Akiangazia ukuaji wa uchumi wa kidijitali na kujizatiti kuchochea matumizi katika manunuzi na kuboresha mazingira ya biashara, Yin ametoa ripoti ya kazi ya serikali katika mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la Manispaa ya Beijing siku ya Jumapili.
Viashiria vya uchumi vinavyolengwa vya mji mkuu huo wa China kwa Mwaka 2024 pia vinajumuisha kudumisha kiwango cha ukosefu wa ajira mijini ndani ya asilimia 5 na kuhakikisha kiwango cha jumla cha bei za matumizi ya wakazi (CPI) unabakia kuwa karibu asilimia 3. Zaidi ya hayo, mapato yatokanayo na bejeti ya jumla ya umma yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 5 mwaka hadi mwaka. Yin amesisitiza dhamira ya Mji wa Beijing kuweka ukuaji wa mapato ya wakaazi kuendana na hali ya upanuzi wa jumla wa uchumi.
Mwaka 2023, Pato la Mji wa Beijing (GDP) liliongezeka hadi karibu yuan trilioni 4.4 (kama dola za Kimarekani bilioni 618.26), ikionyesha ukuaji thabiti wa mwaka hadi mwaka wa asilimia 5.2, inasomeka ripoti hiyo ya kazi ya serikali.
Kati ya mambo yaliyochangia kwa kiwango kikubwa kwenye GDP ya Beijing ni uchumi wa kidijitali, ambao umechangia asilimia 42.9 mwaka 2023. "Beijing inaweka jitihada katika kujijenga kuwa mji wa kimataifa wa mfano katika uchumi wa kidijitali," amesema Yin.
Watu wakichagua maua kwenye duka mjini Beijing, China, Januari 1, 2023. (Xinhua/Ren Chao)
Gari la majaribio lililo na mfumo wa kujiendesha bila madereva likijiendesha kwenye barabara maalum katika Eneo la Zhongguancun mjini Beijing, China, Julai 3, 2020. (Xinhua/Ren Chao)
Takwimu zinaonyesha kuwa matumizi ya jumla kwenye masoko ya Beijing yaliongezeka kwa asilimia 10.2 mwaka hadi mwaka 2023, huku jumla ya mauzo ya bidhaa za matumizi zinazouzwa kwa bei ya rejareja yakifikia yuan trilioni 1.45, sawa na ongezeko la asilimia 4.8 mwaka hadi mwaka.
Sehemu ya pili ya mradi wa jengo la Kituo cha Mambo ya Fedha cha Nanjing wawekewa vifuniko
Umoja wa Mataifa kuchapisha stempu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa 2024
Watu wa sehemu mbalimbali za China wajiandaa kwa Mwaka Mpya kwa kalenda ya jadi ya China
Pilikapilika za uvuvi wa majira ya baridi katika Mkoa wa Hunan, Katikati ya China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma