久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Biashara na?uwekezaji ni muhimu kwa uchumi?wa dunia kuendelea kufufuka: WEF

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2024

Watu wakitembea kuipita nembo ya Baraza la Uchumi Duniani (WEF) mjini Davos, Uswisi, Januari 15, 2024. (Xinhua/Lian Yi)

Watu wakitembea kuipita nembo ya Baraza la Uchumi Duniani (WEF) mjini Davos, Uswisi, Januari 15, 2024. (Xinhua/Lian Yi)

DAVOS, Uswisi - Biashara na uwekezaji bado ni muhimu kwa uchumi wa Dunia kuendelea kufufuka, washiriki wamesema katika Mkutano wa 54 wa kila Mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) unaoendelea mjini Davos, Uswisi.

"Bila ya mtiririko huria wa biashara, sidhani kama tunaweza kufufuka," Ngozi Okonjo-Iweala, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), amesema katika kipindi cha mjadala kilichoangazia mchango wa biashara na uwekezaji katika kuchochea ukuaji wa uchumi.

Akisisitiza uhusiano wa pande mbili kati ya ukuaji wa uchumi na biashara, amesema WTO inajadiliana na nchi 110 kuhusu makubaliano ya kurahisisha uwekezaji, ili kuzisaidia nchi zinazoendelea "kuondoa vikwazo" kwa ajili ya uwekezaji kuingia na kuimarisha tena biashara na ukuaji wa uchumi.

Kwa mujibu wa Okonjo-Iweala, WTO "haikukuwa na matumaini makubwa" kuhusu makadirio ya awali ya ukuaji wa biashara ya bidhaa kwa asilimia 3.3 mwaka huu kutokana na mvutano katika Bahari Nyekundu na kushuka kwa ukuaji wa uchumi duniani.

"Tunayafanyia marekebisho, lakini sina takwimu mpya," amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Ngozi Okonjo-Iweala akizungumza kwenye Mkutano wa 14 wa kila Mwaka wa Vinara Wapya, unaojulikana pia kwa jina la Summer Davos, mjini Tianjin, Kaskazini mwa China, Juni 27, 2023. (Xinhua/Li Xin)

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Ngozi Okonjo-Iweala akizungumza kwenye Mkutano wa 14 wa kila Mwaka wa Vinara Wapya, unaojulikana pia kwa jina la Summer Davos, mjini Tianjin, Kaskazini mwa China, Juni 27, 2023. (Xinhua/Li Xin)

Viongozi wa biashara duniani kote katika WEF wanaona fursa muhimu za uwekezaji kwenye ukuaji wa uchumi katika minyororo ya usambazaji wa bidhaa ya kimataifa, kama vile biashara ya kidijitali, huduma na biashara ya kijani.

Mabadiliko ya fikra yanahitajika, ambapo biashara na utandawazi "vitakumbatiwa kisiasa," amesema Khaldoon Khalifa Al Mubarak, Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mkuu katika Kampuni ya Uwekezaji ya Mubadala ya Falme za Kiarabu.

Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis amesema kuwa kukosekana kwa utulivu wa siasa za kijiografia pia kunaleta hatari kwa minyororo ya usambazaji wa bidhaa na biashara ya kimataifa.

Amesema muktadha wa siasa za kijiografia unabadilika na kuwa wenye migogoro zaidi, na kusababisha hatari ya kugawanyika kwa uchumi.

Chini ya kaulimbiu isemayo "Kujenga Upya Uaminifu," mkutano wa kila mwaka wa WEF, uliopangwa kufanyika Januari 15-19, unatilia maanani vipaumbele vinne: kufikia usalama na ushirikiano katika Dunia iliyogawanyika; kuongeza ukuaji wa uchumi na ajira kwa zama mpya; kutumia kikamilifu teknolojia za akili bandia kama nguvu ya kuendesha uchumi na jamii, na kuunda mkakati wa muda mrefu wa tabia nchi, mazingira ya asili na nishati.

Picha iliyopigwa Januari 10, 2024 ikionyesha gati la kontena la Bandari ya Rizhao mjini Rizhao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua/Guo Xulei)

Picha iliyopigwa Januari 10, 2024 ikionyesha gati la kontena la Bandari ya Rizhao mjini Rizhao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua/Guo Xulei)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>