Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China asema China siku zote itaunga mkono ushirkiano wa pande nyingi
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria Mkutano wa Kila Mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) Mwaka 2024 na kutoa hotuba kwenye mkutano huo mjini Davos, Uswisi, Januari 16, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)
DAVOS, Uswisi – China kamwe haijitoi katika makubaliano au kujiondoa kutoka kwenye mashirika, wala haizitaki nchi nyingine kuchagua upande, na muda wote inaunga mkono ushirikiano wa pande nyingi, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema mjini Davos, Uswisi siku ya Jumanne kwenye Mkutano wa Baraza la Uchumi la Dunia (WEF) Mwaka 2024 na kuongeza kuwa kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu, "Kujenga Upya hali ya Kuaminiana," inawakilisha ufuatiliaji wa watu duniani.
“Kuaminiana kunatoka kwenye matarajio yetu ya pamoja ya mustakabali mzuri wa binadamu na kutokana na nia yetu ya pamoja ya kufanya kazi pamoja kwa ajili yake,” Waziri Mkuu Li amesema alipokuwa akitoa hotuba kwenye hafla iliyoandaliwa na Klaus Schwab, mwanzilishi na mwenyekiti mtendaji wa WEF.
Kama alivyosema Rais Xi Jinping wa China, Dunia imeingia katika kipindi kipya cha misukosuko na mageuzi, lakini mwelekeo wa jumla wa maendeleo na hatua za maendeleo ya binadamu hautabadilika, mienendo ya jumla ya historia ya Dunia inayosonga mbele huku kukiwa na misukosuko na mambo mapya na mwelekeo wa jumla kuelekea mustakabali wa pamoja wa jumuiya ya kimataifa hautabadilika, amesema waziri mkuu Li.
Pande zote zinapaswa kutupilia mbali chuki, kupunguza migawanyiko, kutendeana kwa udhati, kusonga mbele kwa pamoja, na kushirikiana kushughulikia upungufu wa hali ya kuaminiana, amesema Waziri Mkuu wa China.
Ametoa pendekezo lenye vipengele vitano kuhusu kujenga upya hali ya kuaminiana, kuimarisha ushirikiano na kuhimiza kuimarika tena kwa uchumi wa Dunia, ambapo pendekezo la kwanza likiwa ni kuimarisha uratibu wa sera za uchumi wa jumla. Mengine ni kuimarisha mgawanyo wa nguvu kazi wa kimataifa na uratibu wa viwanda, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa kuhusu sayansi na teknolojia, ushirikiano katika maendeleo ya kijani unapaswa kuimarishwa, na kuimarisha ushirikiano wa Kaskazini-Kusini na ushirikiano wa Kusini-Kusini, kutekeleza kikamilifu Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 ya Maendeleo Endelevu.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria Mkutano wa Kila Mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) Mwaka 2024 ulioratibiwa na Klaus Schwab, mwanzilishi na mwenyekiti mtendaji wa WEF, mjini Davos, Uswisi, Januari 16, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma