Lugha Nyingine
Mji wa Beijing, China?wazindua magari yanayojiendesha yenyewe ya kufanya doria barabarani
Mji wa Beijing, China ukizindua rasmi majaribio ya barabarani ya magari yanayojiendesha yenyewe ya kufanya doria, tarehe 16, Januari. (Picha na Zhang Zhang/Xinhua)
Tarehe 16, Januari, Ofisi ya Eneo la Kielelezo la Magari ya Kujiendesha kwa Kiwango cha Juu katika mji wa Beijing, China ilitoa taarifa ya majaribio barabarani, na kuanza rasmi majaribio ya barabarani ya magari yanayojiendesha yenyewe ya kufanya doria. Magari 15 yanayojiendesha yenyewe ya doria yaliwasha taa za tahadhari na kujiendesha kwenye barabara za kawaida za umma moja baada ya lingine. Yameanza kufanya doria ya saa zote 24 za siku bila kusita, na majukumu yao ni kufanya doria na kudhibiti usalama, kulinda usalama wa shughuli zenye watu wengi, kutangaza matangazo kwa umma na kutoa tahadhari, kufanya uokoaji wa dharura n.k.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma