Lugha Nyingine
Wataalamu wakutana nchini Kenya kuhimiza biashara chini ya AfCFTA
Wataalam wanaendelea na mkutano wa siku tatu mjini Nairobi ili kuhimiza biashara chini ya Makubaliano ya Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA).
Mkutano huo wa kwanza wa mikakati ya utekelezaji wa AfCFTA umewakutanisha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, pamoja na maofisa wa serikali kutoka nchi zaidi ya 40 za Afrika ili kupitia upya njia za kufanya biashara huria katika bara hilo.
Mkurugenzi wa kitengo cha ushirikiano wa kikanda na biashara katika Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Afrika (UNECA) Bw. Stephen Karingi, amesema kwenye hotuba yake ya ufunguzi kwamba AfCFTA inashikilia ahadi kwa Bara la Afrika kuondokana na kasumba ya ukoloni ya kuwa masoko madogo na yaliyogawanyika na badala yake kuunda soko moja kubwa lenye watu zaidi ya bilioni 1.4.
Bwana Karingi amesema soko moja la bara linatarajiwa kuunda kiwango cha kuvutia uwekezaji mkubwa wa minyororo ya thamani ya kikanda, na ukuaji wa viwanda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma