久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Mkutano wa kila Mwaka wa WEF wahimiza ushirikiano wakati kukiwa na hali ya kutokuwa na uhakika katika uchumi duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 16, 2024

Watu wakitembea kuipita nembo ya Baraza la Uchumi Duniani (WEF) mjini Davos, Uswizi, Januari 14, 2024. (Xinhua/Lian Yi)

Watu wakitembea kuipita nembo ya Baraza la Uchumi Duniani (WEF) mjini Davos, Uswizi, Januari 14, 2024. (Xinhua/Lian Yi)

DAVOS, Uswisi - Baraza la Uchumi Duniani (WEF) limetoa wito siku ya Jumatatu wa kuimarishwa kwa ushirikiano wa kimataifa, ili kukidhi matakwa ya hali ya kutokuwa na uhakika katika uchumi ambapo wachumi wakuu zaidi ya nusu wamesema kwenye mtazamo wao wa mwaka huu, uliotolewa katika Mkutano wa 54 wa kila mwaka wa WEF, kwamba wanakadiria uchumi wa Dunia kudhoofika Mwaka 2024. Wakati huo huo, wachumi hao saba kati ya 10 wamesema kasi ya mgawanyiko wa uchumi wa kijiografia itaongezeka.

Saadia Zahidi, Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF), akizungumza katika mahojiano kwenye makao makuu ya WEF mjini Geneva, Uswisi, Mei 1, 2023. (Xinhua/Lian Yi)

Saadia Zahidi, Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF), akizungumza katika mahojiano kwenye makao makuu ya WEF mjini Geneva, Uswisi, Mei 1, 2023. (Xinhua/Lian Yi)

"Hali ya kutokuwa na uhakika ni neno la msingi kwa uchumi wa nchi nyingi duniani, ikiwa ni pamoja na China. Habari njema ni kwamba China ni moja ya nchi chache sana zenye uchumi mkubwa duniani ambazo hazikabiliani na mfumuko wa bei, hazisumbuki na viwango vya juu vya riba kwa sasa," alisema Saadia Zahidi, Mkurugenzi Mtendaji wa WEF.

Katika hali ya kuongezeka kwa mgawanyiko wa kiuchumi na hali ya kutokuwa na uhakika duniani, Mkutano wa 54 wa kila mwaka wa WEF umekusanya viongozi kutoka duniani kote kwa ajili ya wiki ya mazungumzo yenye lengo la kuimarisha ushirikiano na kujenga ushirika.

Chini ya kaulimbiu ya "Kujenga upya Hali ya Kuaminiana," mkutano huo utatilia maanani vipaumbele vinne: kufikia usalama na ushirikiano katika Dunia iliyotengana; kuongeza ukuaji wa uchumi na nafasi za ajira katika zama mpya; kutumia kikamilifu teknolojia za akili bandia kama nguvu ya kuendesha uchumi na jamii, na kuunda mkakati wa muda mrefu wa tabianchi, mazingira ya asili na nishati.

Klaus Schwab, Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa WEF, amesisitiza udharura wa kujenga upya hali ya kuaminiana katika Dunia iliyogawanyika zaidi. Amesisitiza haja ya kwenda mbele zaidi ya udhibiti wa majanga na kushughulikia sababu zake za kimsingi.

Picha hii iliyopigwa Januari 14, 2024 ikionyesha mandhari ya nje ya Kituo cha Mikutano cha Mkutano wa kila Mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) Mwaka 2024 mjini Davos, Uswizi. (Xinhua/Lian Yi)

Picha hii iliyopigwa Januari 14, 2024 ikionyesha mandhari ya nje ya Kituo cha Mikutano cha Mkutano wa kila Mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) Mwaka 2024 mjini Davos, Uswizi. (Xinhua/Lian Yi)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>