Lugha Nyingine
Kampuni ya Magari ya BMW yaripoti ongezeko kubwa la mauzo ya magari yanayotumia umeme nchini China
Magari yanayotumia umeme aina ya i3 ya Kampuni ya magari ya BMW yakionekana kwenye Kiwanda cha Lydia cha Kampuni ya Magari ya BMW Brilliance (BBA) katika Eneo la Tiexi la Mji wa Shenyang, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China, Juni 23, 2022. (Xinhua/Yang Qing)
SHENYANG - Kundi la kampuni za magari za BMW limeuza na kuwasilisha kwa wateja magari 99,972 yanayotumia umeme kikamilifu katika soko la China Mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia zaidi ya 138 kuliko mwaka jana, kampuni hiyo ya kuunda magari imesema na kuongeza kuwa, ongezeko hilo la kasi la mauzo ya magari hayo yanayotumia nishati mpya nchini China limehamasisha mahitaji ya vifaa vya kuchaji na vifaa vya nyongeza.
Hadi kufikia mwisho wa Mwaka 2023, vituo vya kuchaji vya kiumma vya BMW vimefikia zaidi ya 580,000 katika miji zaidi 320 nchini China.
Mwezi Agosti, 2023, BMW ilianzisha mpango wa kujenga kituo kikubwa zaidi cha kuchaji chenye nishati ya umeme inayofikia kilowati 600 ili kusaidia vituo vya kuchaji vyenye nguvu kubwa.
Hadi kufikia mwisho wa Mwaka 2023, vituo 50 vya aina hiyo vilikuwa vimejengwa nchini China, vikipatikana katika miji 17 ya daraja la kwanza na la pili.
Mwaka 2023, Kundi la kampuni za magari za BMW liliuza na kuwasilisha kwa wateja magari ya BMW na MINI jumla ya zaidi ya 820,000 katika soko la China.?
Wanasarakasi wa China waonekana kwenye Tamasha la Kimataifa la Sarakasi la Budapest, Hungary
Treni ya tramu inayotumia umeme yapambwa na taa ili kuvutia watalii huko Dalian, China
Taa za kupendeza za mapambo zaleta shamrashamra za mwaka mpya mkoani Shandong, China
Ukaushaji wa mahindi waleta mandhari kama ya picha ya kuchorwa katika Mji wa Mile, Yunnan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma