Lugha Nyingine
Faharisi ya kiwango cha usafirishaji wa bidhaa kwenye pwani za China yaongezeka Mwezi Desemba, 2023
Picha hii iliyopigwa Desemba 27, 2023 ikionyesha gati la kiotomatiki la Bandari ya Qingdao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Picha na Zhang Jingang/Xinhua)
SHANGHAI--Faharisi ya kiwango cha usafirishaji wa bidhaa kwenye pwani za China ilipanda kwa asilimia 11.9 Mwezi Desemba 2023 kuliko mwezi uliotangulia, takwimu kutoka Idara ya Biashara ya Usafirishaji ya Shanghai (SSE) zimeonyesha, na mwezi wa Desemba faharisi jumuishi ya kiwango hicho katika maeneo ya pwani, ambayo hupima gharama za usafirishaji katika soko la usafirishaji wa meli wa pwani, ilikuwa 1,135.21.
Katika kipindi hicho, faharisi ndogo kwa usafirishaji wa makaa ya mawe ilipata ongezeko kubwa zaidi la asilimia 15.8 kuliko kipindi kama hiki cha mwaka uliopita, ikifuatiwa na ile ya nafaka na madini ya chuma.
Faharisi ndogo ya mafuta ghafi iliongezeka kwa asilimia 0.5 kuliko mwezi uliopita, wakati ile ya mafuta yaliyosafishwa iliongezeka kwa asilimia 2 kwa mwezi.
SSE ilianzisha utoaji wa faharisi hiyo Mwaka 2001 chini ya uongozi wa Wizara ya Usafirishaji na Uchukuzi ya China ili kuakisi kikamilifu mabadiliko ya soko la usafirishaji wa pwani la China.?
Wanasarakasi wa China waonekana kwenye Tamasha la Kimataifa la Sarakasi la Budapest, Hungary
Treni ya tramu inayotumia umeme yapambwa na taa ili kuvutia watalii huko Dalian, China
Taa za kupendeza za mapambo zaleta shamrashamra za mwaka mpya mkoani Shandong, China
Ukaushaji wa mahindi waleta mandhari kama ya picha ya kuchorwa katika Mji wa Mile, Yunnan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma