Lugha Nyingine
Thamani ya Shilingi ya Kenya dhidi ya Dola ya Marekani yaendelea kushuka
Thamani ya Shilingi ya Kenya imeendelea kupungua na kufikia shilingi 160 dhidi ya Dola moja ya Marekani, na hivyo kutoa shinikizo kwa akiba ya fedha za kigeni ya Kenya na kuongeza gharama ya uagizaji bidhaa kutoka nje.
Benki Kuu ya Kenya (CBK) imesema kuwa, kwenye biashara ya siku ya Alhamisi, thamani ya sarafu ya nchi hiyo dhidi ya dola moja ilikuwa ikibadilishwa kwa shilingi 159.8 ikiwa ni kushuka kwa takriban asilimia 27 kwa mwaka hadi sasa.
Hadi kufikia Januari 5, akiba ya fedha za kigeni ya Kenya ilikuwa chini ya dola bilioni 6.78, sawa na akiba ya miezi 3.62 tu ya malipo ya uagizaji, ikiwa imepungua kwa takriban dola bilioni 1 kwa mwaka.
Kuporomoka huko kwa thamani ya shilingi ya Kenya kumetajwa kuwa ni kutokana na kasi ya kubana sera ya fedha kwenye nchi zilizoendelea, ambako kumesababisha kupungua kwa mapato.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma