Lugha Nyingine
China yawa?soko kubwa zaidi la biashara za rejareja za mtandaoni duniani kwa miaka 11 mfululizo
Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Shu Jueting tarehe 11 kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema kuwa, China imekuwa soko kubwa zaidi la biashara za rejareja za mtandaoni duniani kwa miaka 11 mfululizo.
Takwimu zinaonesha kuwa, thamani ya jumla ya miamala ya biashara za mtandaoni za China imeongezeka kutoka Yuan trilioni 31.63 (takriban Dola za Marekani trilioni 4.42) mwaka 2018 hadi Yuan trilioni 43.83 (takriban Dola za Marekani 6.12) mwaka 2022. Mauzo ya bidhaa zinazoshikika kwenye mtandao yanachukua zaidi ya robo ya mauzo ya jumla ya bidhaa za rejareja. Katika miaka mitano iliyopita, watu walioshughulikia biashara mtandaoni waliongezeka kutoka milioni 47 hadi zaidi ya milioni 70.
Ushirikiano wa kimataifa katika biashara ya mtandaoni ya China nao unaongezeka kwa kina hatua kwa hatua. China imeanzisha eneo la majaribio la ushirikiano wa “biashara za mtandaoni wa Njia ya Hariri” katika Mji wa Shanghai, ili kupanua ufunguaji mlango katika sekta ya biashara ya mtandaoni.
Tarehe 1, Januari mwaka huu ilitimia miaka mitano tangu kutekelezwa kwa “Sheria ya Biashara za Mtandaoni ya Jamhuri ya Watu wa China”. Shu amesema, tangu kutekelezwa kwa sheria hiyo Mwaka 2019, mazingira ya biashara ya mtandaoni ya China yameboreshwa siku hadi siku, na biashara ya mtandaoni imekuwa sehemu muhimu katika uchumi wa kidijitali, ambayo ni yenye ukubwa zaidi wa maendeleo, kuhusisha maeneo makubwa zaidi na yenye shughuli nyingi zaidi za ujasiriamali na uvumbuzi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma