Lugha Nyingine
Sekta ya Usambazaji wa Bidhaa ya China Yapanuka kwa haraka mwezi Desemba
Mashine ikipakia kontena lenye shehena ya mzigo kwenye kituo cha ushirikiano wa uchukuzi wa China-Kazakhstan katika Bandari ya Lianyungang ya Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, Mei 9, 2023. (Xinhua/Liu Wenhui)
BEIJING – Takwimu zilizotolewa na Shirikisho la Usambazaji na Ununuzi wa Bidhaa la China (CFLP) zimeonesha kuwa, sekta ya usambazaji wa bidhaa ya China imerekodi upanuzi wa haraka Mwezi Desemba, ambapo faharisi ya kufuatilia ufanisi wa soko la usambazaji wa bidhaa la China ilifikia asilimia 53.5 mwezi uliopita, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.2 kuliko ile ya Mwezi Novemba.
Faharisi ya asilimia zaidi ya 50 inaonyesha upanuzi, wakati ile ya chini ya hiyo inaonyesha kudorora.
Mwanauchumi mkuu wa CFLP He Hui amesema sekta hiyo imeripoti kuboreshwa kwa nguvu ya uhai ya sekta hiyo mnamo Desemba kutokana na mahitaji mapya ya wanunuzi yanayodumisha mwelekeo wa juu na biashara zikishikilia matarajio thabiti kwa ukuaji wa siku zijazo.
Katika uchanganuzi huo, faharisi ndogo zinazopima kiasi cha jumla cha biashara na oda mpya za usambazaji wa bidhaa ilikuwa asilimia 53.5 na asilimia 52.8, mtawalia, na ile ya matarajio ya biashara ilifikia asilimia 54.8.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma