Lugha Nyingine
Uchumi wa Kenya wakadiriwa kukua kwa asilimia 5.5 mwaka 2024
(CRI Online) Desemba 21, 2023
Wizara ya Fedha ya Kenya imesema kuwa uchumi wa nchi hiyo utakua kwa asilimia 5.5 mwaka 2024.
Wizara hiyo imesema katika taarifa yake ya sera ya bajeti kwa mwaka 2024 kwamba ukuaji wa uchumi utaungwa mkono na ukuaji endelevu wa sekta za huduma, kuimarika kwa sekta ya kilimo, na utekelezaji wa hatua za kuhamasisha shughuli za kiuchumi katika sekta za kipaumbele zilizotajwa na serikali.
Taarifa hiyo imesema uchumi unatarajiwa kuendelea kukua kwa uthabiti na kuongezeka kwa asilimia 5.5 mwaka 2023 na 2024, na asilimia 5.4 mwaka 2025.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma