Lugha Nyingine
Benki?Kuu Tanzania yasema Ufanisi wa uchumi wa Tanzania kwa mwaka 2023 ulikuwa?wa kuridhisha
Benki kuu ya Tanzania imesema ufanisi wa uchumi wa Tanzania kwa mwaka 2023 ulikuwa wa kuridhisha licha ya athari za mshtuko wa dunia.
Benki hiyo imesema katika taarifa yake iliyotolewa Jumanne kuwa mwaka kesho wa 2024 ufanisi wa uchumi unatarajiwa kuimarika kutokana na utekelezaji wa sera za kuchochea ukuaji na kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi.
Ukuaji katika robo ya kwanza na ya pili ya mwaka 2023 ulikuwa asilimia 5.4 na asilimia 5.2 mtawalia, ukiimarishwa na uwepo wa aina mbalimbali za shughuli za kiuchumi. Ukuaji katika shughuli za kiuchumi pia umeshuhudiwa kwa upande wa Zanzibar, kutokana na kuimarika kwa utalii na uwekezaji wa umma na binafsi.
Habari pia zinasema Benki ya Dunia tawi la Tanzania imeipongeza Tanzania kwa kuwa na ongezeko imara la kiuchumi na kuzipita nchi nyingi zinazoendelea, lakini benki hiyo imesema Tanzania inatakiwa kujikita zaidi kwenye sekta binafsi ili kuwa na ukuaji zaidi katika miaka ijayo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma