Lugha Nyingine
Tanzania yatajwa kuwa moja ya maeneo yanayovutia zaidi kibiashara
Tanzania imejijengea nafasi muhimu katika biashara barani Afrika kutokana na uhusiano na nchi nyingi duniani, hivyo kuwa na uwezo wa kifursa katika kupata nafasi ya kuanzisha na kuendeleza viwanda.
Akiongea mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya EnergyNet, Bw. Simon Gosling amesema Tanzania ni eneo muhimu kwa shughuli za uwekezaji barani Afrika, ambapo inajiandaa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa tano wa Kilele wa Ushirikiano wa Nishati wa Tanzania (5th Tanzania Energy Cooperation Summit -TECS) unaotarajiwa kufanyika kuanzia Januari 31 hadi Februari 2024 mjini Arusha.
Amesema kwa kuzingatia nafasi ya Tanzania kama mhimili wa nishati wa kikanda, mada zitakazojadiliwa katika mkutano huo zitakuwa ni pamoja na mtazamo wa kiuchumi wa Tanzania na uwezo wa maendeleo ya nishati, pamoja na kupanga njia bora ya kujenga soko la umeme la kikanda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma