Lugha Nyingine
Mkutano wa kazi ya uchumi ya Kamati Kuu ya CPC wafanyika mjini Beijing (2)
(CRI Online) Desemba 13, 2023
(Picha inatoka shirika la habari la China Xinhua.) |
Mkutano wa kazi ya uchumi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefanyika mjini Beijing ambapo Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati ya Kijeshi ya China ya Kamati Kuu Xi Jinping amehudhuria na kutoa hotuba muhimu.
Katika hotuba yake Rais Xi amefanya majumuisho kwa pande zote kazi ya uchumi ya mwaka 2023, kuchambua kwa kina hali ya hivi sasa ya kiuchumi, na kuweka majukumu ya uchumi ya mwaka 2024.
Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Waziri Mkuu wa China Li Qiang alitoa hotuba akifanya majumuisho ya kazi na kutoa matakwa ya kutekeleza maagizo aliyotoa Rais Xi katika hotuba yake na majukumu ya uchumi ya mwaka ujao.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma