Lugha Nyingine
Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Vietnam wanufaisha watu wa nchi zote?mbili
Wafanyabiashara wa Vietnam wakiuza matunda ya madoriani katika Eneo la Maonyesho ya Bidhaa za ASEAN la Maonesho ya 20 ya China-ASEAN. (Picha na Zhang Ailin/Xinhua)
Mwaka huu ni maadhimisho ya kutimia miaka 15 tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Vietnam. China na Vietnam zinaharakisha ujenzi wa pamoja wa Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na "Kanda Mbili na Mzunguko Mmoja", zikitumia kikamilifu mazingira wezeshi ya muunganisho, zikifanya jitihada kuweka minyororo ya viwanda na ugavi imara na laini, zikidumisha kuboresha kiwango cha ushirikiano wa kiuchumi na uwekezaji wa kibiashara, na kuendeleza maendeleo yenye ubora wa juu ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara. Ili kuhudumia vizuri zaidi ustawi wa watu wa nchi hizo mbili, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili umepata mafanikio yenye matunda mazuri.
Biashara kati ya China na Vietnam yaendelea kwa kasi
Katika miaka ya hivi karibuni, biashara ya pande mbili kati ya China na Vietnam imeendelea kwa kasi. Kiwango cha biashara baina ya nchi mbili kimeongezeka kutoka dola za kimarekani zaidi ya bilioni 2.4 mwaka 2000 hadi dola za kimarekani zaidi ya bilioni 234.9 mwaka 2022. China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Vietnam kwa miaka mingi, na Vietnam ni mshirika mkubwa zaidi wa biashara wa China katika Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) na mshirika mkubwa wa nne wa kibiashara duniani.
"Miundo ya bidhaa za kuagiza na kuuza nje ya China na Vietnam inaendana sana, na kiwango cha biashara kinaendelea kufikia viwango vipya, na kunufaisha watu wa nchi mbili." Xu Liping, mtafiti wa Taasisi ya Asia-Pasifiki na Mkakati wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Jamii cha China, amesema huku akiongeza kwamba ukubwa wa biashara unaendelea kuongezeka, hali inayoonyesha uhai wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Vietnam.
Ushirikiano wa uwekezaji umepata matokeo ya ajabu
Katika miaka ya hivi karibuni, kampuni za kibiashara za China zimeongeza kwa kiasi kikubwa uwekezaji wao nchini Vietnam, na uwiano wao wa uwekezaji wa kigeni nchini Vietnam umeongezeka mwaka hadi mwaka. Ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na Vietnam umepata matokeo ya dhahiri. Kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, uwekezaji wa moja kwa moja wa kampuni za China katika sekta nzima ya Vietnam ulifikia dola za Kimarekani bilioni 1.76, ambayo inaendana na mahitaji ya mageuzi na uboreshaji wa kiuchumi wa Vietnam. Uwekezaji katika teknolojia ya hali ya juu, mawasiliano ya habari, nishati mpya, maendeleo ya kijani, biashara ya mtandaoni na usafirishaji wa biashara na nyanja zingine umeongezeka sana, huku ukiwa na uwezo mkubwa wa kifursa.
Xiong Bo, Balozi wa China nchini Vietnam, amesema China na Vietnam ziko katika hatua muhimu ya maendeleo yao. Amesema, upande wa China uko tayari kuimarisha ushirikiano wa uwekezaji, kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili, kuimarisha ushirikiano katika uwezo wa uzalishaji viwandani, kusukuma ushirikiano wa kivitendo kati ya nchi hizo mbili katika nyanja za uchumi wa kidijitali, uchumi wa kijani, nishati mpya, miundombinu n.k., na kuiunga mkono Vietnam kuharakisha mchakato wake wa maendeleo ya kiviwanda.
Ushirikiano wa kikanda unaendelea kuimarika
Katika miaka ya hivi karibuni, China na Vietnam zimeshikilia kanuni ya mashauriano ya kina, mchango wa pamoja na kuchangia manufaa, zikitumia kikamilifu faida zao za ukaribu wa kijiografia na kuendana kiviwanda, kuharakisha ujenzi wa pamoja wa Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na " Korido Mbili na Mzunguko Mmoja", na kujikita katika kuhimiza ushirikiano katika maeneo ya kimkakati kama vile muunganisho.
Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh alisema upande wa Vietnam unathamini uhusiano wa kirafiki na kindugu na China, unathamini sana matokeo ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili, na uko tayari kushirikiana na China kuimarisha "Kanda Mbili na Mzunguko Mmoja" na ujenzi wa pamoja wa Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuhimiza ushirikiano wa muunganisho wa reli na kuboresha ufunguaji mlango wa bandari za mipakani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma