Lugha Nyingine
Marais wa China na Belarus waahidi kuimarisha uhusiano
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko mjini Beijing, China, Desemba 4, 2023. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko mjini Beijing siku ya Jumatatu ambapo ameeleza kwamba yeye na Lukashenko walifikia makubaliano muhimu juu ya maendeleo ya kiwango cha juu ya uhusiano wa China na Belarus wakati wa ziara ya kiserikali ya Lukashenko nchini China mwishoni mwa Mwezi Februari mwaka huu na kwamba nchi hizo mbili zimeimarisha hali ya kuaminiana kisiasa na uratibu wa mambo ya kimataifa tangu wakati huo.
Amesema, China daima inautazama uhusiano wake na Belarus kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, inaiunga mkono kithabiti Belarus katika kufuata njia ya maendeleo inayoendana na hali ya nchi yake, na inapinga uingiliaji wa nje katika masuala ya ndani ya Belarus.
"China iko tayari kuendelea kuimarisha uratibu wa kimkakati na Belarus, kusaidiana kithabiti, kuongeza ushirikiano wa kivitendo na kuimarisha uhusiano wa pande mbili," Rais Xi amesema.
Amesisitiza kuwa zaidi ya nchi 150 zimeshiriki kwenye ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja muongo mmoja baada ya yeye kutoa pendekezo hili, na muda si mrefu alitangaza hatua nane ambazo China itachukua ili kuunga mkono ujenzi wa pamoja wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja. "China inaikaribisha Belarusi kuendelea kushiriki kikamilifu na kupata fursa zaidi za maendeleo halisi kutoka kwake."
Amesema pande hizo mbili zinapaswa kupanua ushirikiano katika sekta za elimu, afya, michezo na utalii, kusaidia mawasiliano na ushirikiano kati ya vijana, na kuimarisha maelewano na urafiki kati ya nchi hizo mbili.
Akieleza kuwa China na Belarus ni nguvu muhimu katika mageuzi na maendeleo ya mfumo wa usimamizi wa kimataifa, Rais Xi amesema China iko tayari kuimarisha uratibu na ushirikiano na Belarus ndani ya mifumo ya pande nyingi.
Kwa upande wake Lukashenko amesema chini ya uongozi wa Rais Xi, China imepata mafanikio makubwa katika maendeleo yake na zaidi ya watu bilioni 1.4 wa China wanaishi maisha ya furaha, na kutoa mchango muhimu kwa Dunia.
Lukashenko amesema, “Belarus inatumai kwa dhati kuwa China itaimarika, jambo ambalo linafaa kwa amani na maendeleo duniani,” na nchi yake iko tayari kushirikiana na China katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uratibu wa mambo ya kimataifa.
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko mjini Beijing, China, Desemba 4, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma