Lugha Nyingine
Kituo cha biashara kilichojengwa na kampuni ya China nchini Tanzania chatoa ajira na kukuza uchumi
(CRI Online) Desemba 01, 2023
Kituo cha biashara na ugavi kilichojengwa na kampuni ya China nchini Tanzania ambacho kimepangwa kufunguliwa kwa majaribio mwezi Julai mwaka 2024 nchini Tanzania, kimetoa maelfu ya nafasi za ajira kwa wenyeji na kinatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.
Mradi wa Kituo cha Biashara na Ugavi cha Afrika Mashariki chenye eneo la ukubwa wa mita za mraba 75,000 kwa ajili ya maduka elfu mbili pamoja na maegesho, unafadhiliwa na Kampuni ya Kituo cha Biashara na Ugavi cha Afrika Mashariki (EACLC), ambayo ni kampuni ya China inayojishughulisha na biashara ya kimataifa, na ujenzi wake unatekelezwa na Kampuni ya uhandisi wa ujenzi ya CCECC ya China.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma